Timu ya taifa ya Tanzania kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 maarufu kama Serengeti Boys April 5 2016 ilileta faraja kwa watanzania, baada ya kuendeleza umahiri wake wa kuifunga timu ya taifa ya vijana ya Misri The Pharaohs mara mbili mfululizo.
Serengeti Boys ilirudiana kwa mara ya pili na timu ya taifa ya Misri na kufanikiwa kuifunga kwa jumla ya goli 3-2, ushindi huo unakuja ikiwa ni siku chache zimepita toka Serengeti Boys iwafunge Misri kwa jumla ya goli 2-1, magoli ya leo ya Serengeti Boys yalifungwa na Ibrahim Abdallah dakika ya 28, 60 na Boko Seleman aliyefunga dakika ya 36.
Wakati magoli ya Misri yalifungwa na Ahmed Saad dakika ya 22 na Diaa Wahid aliyefunga goli la pili dakika ya 74, mchezo huo unatajwa kuwa na mvuto na timu zote ziligawana kuutawala mchezo kwani Serengeti ilitawala kipindi cha kwanza.
PICHA KWA HISANI: salehjembe.com
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE
KAMA ULIKOSA KUTAZAMA VIDEO YA GOLI YA LA SAMATTA DHIDI YA CHAD
https://youtu.be/f2pdjFVtoV0