Kwenye dunia ya sasa Wasanii wa muziki pia wanayo nafasi ya kulipwa au kujiingizia pesa kutokana na vyanzo mbalimbali na hiyo yote ni kutokana na muziki wao ndio maana sio kitu kigeni tena kuona msanii analipwa pale nyimbo zake zinapochezwa redioni.
Kama ulikua hujui, mwimbaji staa wa Tanzania Vanessa Mdee huwa anapokea pesa zake mara kwa mara kutokana na nyimbo zake kuchezwa kwenye Radio na TV za Afrika Kusini ambapo hii imekua ni kanuni inayofatwa kwa baadhi ya nchi, Radio na TV kuwalipa wasanii kutokana na jinsi nyimbo zao zilivyochezwa.
Sio kila msanii anaweza kulipwa kama hivyo, kwa Wasanii wanaotoka nje ya nchi kuna vigezo vinatazamwa kukuwezesha kusajiliwa na mamlaka husika na baada ya hapo unakua kwenye mzunguko wa kulipwa kama Wasanii wengine wa nchi hiyo wanavyolipwa.
Vanessa anasema ‘Kwanini Tanzania tusiende juu zaidi? ni kitu kizuri sana hiki…… kuanzia nilipotoa wimbo wa no body but me niliofanya na rapper K.O wa South Africa ndio nimeanza kulipwa sababu nilikua sijajiandikisha kabla ya hapo, South Africa msanii yeyote mziki wake ukichezwa kwenye Radio, TV au migahawani na sehemu nyingine analipwa‘
Kenya kumekua na hii sheria kwa muda sasa hivi ambapo Taxi, Saluni, Baa na sehemu nyingine za public kama club na hotelini wamiliki wake hulazimika kulipia ada ya kila mwaka na kupewa stika maalum kuwaruhusu kucheza muziki wa Kenya.
Diamond Platnumz wa Tanzania ni miongoni mwa Wasanii wanaolipwa nchini Kenya pale nyimbo zao zinapochezwa na hii ni baada ya kujiandikisha ambapo mara ya mwisho Wasanii kama Chege, YamotoBAND walitajwa nyimbo zao kuchezwa sana lakini hawawezi kupewa pesa zao sababu hawakujiandikisha.
ULIKOSA JINSI WATOTO WA KITANZANIA WALIVYOCHEZA MBELE YA VANESSA MDEE BAADA YA KUTANGAZA KUTAFUTA DANCERS? TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE