Mkali wa muziki wa dansi aliyefanya vizuri akiwa na bendi ya FM Academia na Stono Musica, Ndanda Kosovo ambaye alikuwa akisumbuliwa na vidonda vya tumbo ambapo alilazwa katika hospitali ya mwananyamala na baada ya hali yake kuwa mbaya alihamishiwa katika hospitali ya Muhimbili.
April 09 2016 zimeripotiwa habari za kifo chake na millardayo.com imepata nafasi ya kuzungumza na Baba mdogo wa mwanamuziki huyo, Kardinal Gental ambaye amethibisha kifo chake>>>’Ni kweli kabisa ndanda amefariki nilikuwa naye jana muhimbili tangu asubuhi mpaka usiku tumekesha naye pale mpaka leo saa moja asubuhi mke wake alipokuja mimi nikaondoka nikaacha anamlisha lakini baadaye wakanitumia taarifa taarifa kwamba ndanda amefariki’.
>>>>’Kitu kikubwa kilichomuondoa Ndanda ni vidonda vya tumbo kwani alikuwa akitapika mpaka kuna chembechembe za damu zilikuwa zinatoka‘
UNAWEZA KUBONYEZA PLAY HAPA CHINI KUPATA TAARIFA KAMILI YA KIFO CHA NDANDA KOSOVO
UNAWEZA KUSIKILIZA MOJA YA WIMBO WA NDANDA KOSOVO KWA KUBONYEZA PLAY HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE