Kupitia mitandao ya kijamii kulisambaa video fupi ya Dudubaya ambaye ni msanii wa siku nyingi Tanzania akionekana kumtukana matusi ya nguoni msanii Shetta wa bongofleva kisa ni kutokana na msanii huyu Shetta kutumia jina la Mamba.
Baada ya hiyo video kusambaa, Dudubaya amejifikiria na kuona hakufanya kitu sahihi na akalazimika kumuomba Shetta msamaha kupitia Instagram yake na kuandika >>> ‘Kusema ukweli kabisa sikuwa kwenye hali yangu ya kawaida wakati narekodiwa ile video, nilikua nimelewa sana Pombe’
Sasa pamoja na Dudubaya kuomba msamaha, ameongea na AyoTV na kusisitiza kwamba ‘Mimi ni mtoto wa Mungu na nimelelewa na kanisa langu takatifu katoliki la mitume Roman, niliona Shetta ameongea kwenye XXL na kusema aliumia kutukaniwa wazazi wake….‘
‘Baada ya hiyo Interview mimi ndio nikaamua kumuomba msamaha……kwa sababu ya yale maneno mazito niliyoyatumia ila msamaha huu haumaanishi kwamba ndio nimemwachia aendelee kutumia jina la Mamba, hicho ni kitu kingine….. nimemuomba tu msamaha kwa sababu nilimtukania Wazazi wake, wazazi wa Shetta ni wazazi wangu na wazazi wangu ni wazazi wa Shetta‘ – Dudubaya
Unaweza kutazama full story kwenye hii video hapa chini kupata na nyingine kubwa za bongo…
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE