April 17 2016 Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Ufugaji Mwigulu Nchemba aliongozana na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu mpaka kwenye machinjio ya Vingunguti Dar baada ya machinjio hayo kufungiwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA kwa kutozingatia usalama na usafi wa maeneo ya machinjio.
Baada ya kikao cha muda mfupi kilichofanyika kwenye machinjio ya Vingunguti Waziri Nchemba aliyaongea haya ‘Kwanza kuna mambo kadhaa tumeyaona ambayo TFDA wamefanya kazi nzuri sana nawapongeza sana wamebaini ukosefu wa maji, na pia visu vinavyotumika kuchinjia vinasafishwa mahali ambapo sio salama vinasafishwa bafuni‘ >>>Mwigulu Nchemba Waziri wa Kilimo Uvuvi na Ufugaji
”Kwa hiyo nataka kuwatoa hofu watanzania kuwa nyama itakayokuwa kwenye mabucha itakuwa ni nyama salama lakini tutahakikisha tunaendelea kulinda viwango vya nyama ili wasiweze kupata madhara ya kiafya‘>>>Waziri wa Afya Ummy Mwalimu
UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI ILI KUJUA KILE WALICHOKIAMUA KWENYE MACHINJIO YA VINGUNGUTI
ULIIKOSA YA WAZIRI NCHEMBA KUFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA USIKU NA KUMFUKUZA KAZI MKURUGENZI? ANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE