Baada ya headlines za muda mrefu kuhusu hatma ya suala la uchaguzi mkuu wa klabu ya Dar es Salaam Young Africans kupita muda wa kufanyika, April 25 2016 mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa TFF Aloyce Komba ameongea mambo matatu leo.
“Leo kikubwa ninachotaka kukifanya kuhusu uchaguzi mkuu Yanga halafu mengine yatafuata ni kutangaza tarehe ya uchaguzi, rasmi sasa uchaguzi wa Yanga utafanyika June 5 2016 siku ya jumapili” >>> Aloyce Komba
“Lakini tarehe 3 Mei 2016 nitatangaza nafasi zinazogembewa kwa mujibu wa kalenda ya uchaguzi wa Yanga, hata hili nililolifanya la kutangaza tarehe nilitakiwa kutangaza Mei 3 ila hiyo siku nitatangaza nafasi zinazogombewa” >>> Aloyce Komba
“Kwa mujibu wa katiba ya Yanga hadi sasa wanakuwa hawana uongozi na hata kama walikuwa na kamati ya muda ina kufa na kamati yangu ndio inakuwa inashughulikia moja kwa moja” >>> Aloyce Komba
Hayo ni baadhi ya mambo matatu yaliotangazwa na mwenyekiti kamati ya uchaguzi ya shirikisho la soka Tanzania TFF ambayepia ni wakili Aloyce Komba kuhusu uchaguzi mkuu wa Yanga.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE
ALL GOALS: Yanga vs Al Ahly (Full Time 1-1) April 9 2016 CAF
https://youtu.be/VSM0_i0-DY0