Mahakama ya Rufaa imesikiliza rufaa ya kupinga kuachiwa huru kwa aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es salaam ‘RCO’ Kamishna Msaidizi wa Polisi ‘ACP‘ Abdallah Zombe na askari wenzake watatu waliokuwa wanakabiliwa na mashitaka ya mauaji.
Rufaa hiyo imesikilizwa mbele ya jopo la majaji watatu ambapo wamesikiliza pande zote mbili wa mashitaka na utetezi na itatoa maamuzi baada ya majaji kupitia kesi hiyo.
Mkurugenzi wa Mashitaka ‘DPP’ alikata rufaa mwaka 2013 akipinga hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam iliyowaachia huru Zombe na wenzake baada ya kuwaona hawana hatia katika kesi ya mauaji ya watu wanne iliyokuwa inawakabili.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE
ULIIKOSA HII YA ‘KWA NINI TAKUKURU HAWAJAWAFIKISHA HAWA MAHAKAMANI’?-ZITTO, UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI