May 04 2016 Wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo ilitangaza kuufungia wimbo wa Snura ‘chura’ kuchezwa kwenye MEDIA mpaka hapo Snura atakapoifanyia marekebisho video ya wimbo huo na kutoa wimbo huo kwenye mitandao yote ya kijamii.
Leo May 05 2016 Snura Mushi amekutana na waandishi wa habari na kuzungumzia ishu ya kufungiwa wimbo wake wa ‘chura’, mbele ya waandishi wa Habari Snura amewaomba radhi wananchi kwa kutoa nyimbo ya ‘chura’ ambayo imesitishwa na serikali kwa kuiona nyimbo hiyo ina udhalilishaji na haipo kimaadili ya kitanzania.
Snura Mushi ameahidi kutotoa tena video yenye maudhui kama yale na tayari ameruhusiwa kufanya show katika majukwaa mbalimbali baada ya kujisajili baraza la Sanaa la Taifa na kupewa cheti.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE
ULIKOSA SERIKALI WALIPOTANGAZA KUUFUNGIA WIMBO WA SNURA WA ‘CHURA NA VIDEO YAKE? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI