Shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA leo May 6 2016 limeleta barua Tanzania kwa klabu ya Simba na nakala kwa shirikisho la soka Tanzania TFF, barua ambayo inaagiza Simba kulipa pesa za mchezaji wake wa zamani iliyomuacha Donald Musoti bila kumalizia fedha zake za usajili na pesa za kuvunja mkataba baada ya kumuacha.
FIFA imeagiza Simba katika barua yake iliyoandikwa May 3 2016 na kufika Tanzania leo May 6 2016 kumlipa Musoti Tsh milion 64.2 za kitanzania pamoja na gharama ya kikao cha Idara ya Utatuzi wa Migogoro (Desputes Resolution Chamber) cha FIFA.
Miongoni mwa fedha wanazotakiwa kulipa Simba ni Tsh 4,582,000 za fidia, Tsh 1,145,500 ya gharama za kikao cha idara ya migogoro ya FIFA, Musoti aliyesajiliwa na Simba msimu wa 2014/15 na kuachwa alilalamika FIFA kwa kumtumia mwanasheria wake Felix Majani, FIFA ambayo iliona Musoti ana hoja, hivyo Simba imetakiwa kumlipa.
Kiasi kingine anachodai ni Dola 600 (Sh 1,290,000) zilizobaki katika usajili ambapo jumla yake ni Sh 64.2 milioni. Pia Mosoti anamlipa Mwanasheria wake dola 2,000 (Sh 4.3 milioni) kwa ajili ya kusimamia kesi hiyo. Kama Simba itashindwa kulipa deni hilo ndani ya siku 30, itaponywa point tatu au kushushwa daraja.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE
ALL GOALS: SIMBA VS COASTAL UNION FA CUP APRIL 11 2016, FULL TIME 1-2