Mei 10 2016 Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa imewasilisha hotuba yake ya mapitio ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2016/2017 ambayo imesomwa na Waziri wake Hussein Mwinyi.
Katika kipindi cha kuchangia Mbunge wa Kawe Halima Mdee naye alipata nafasi ya kuwasilisha maoni yake kuhusu Wizara hiyo..>>
‘Huu ni mwaka wangu wa kumi na moja bungeni, katika kipindi chote nazungumzia suala la pensheni. Tunaambiwa mtumishi wa Polisi aliyestaafu kipindi cha 2009 kushuka chini analipwa laki moja na tisini kwa mwezi‘
‘Kwa maisha ya sasa hiyi huyu Mwanajeshi anaishije? ninajua Rais ana dhamana ya kuangalia hivi viwango, naomba lifanyiwe kazi‘
‘Leo tunalalamika kuna uharifu wa kibenki, hawa wastaafu wetu tuwaangalie kwa jicho pana. Mwaka 1978-1979 hawa wastaafu wetu walishiriki kwenye vita Uganda, Serikali ya Uganda ilitoa kiinua mgongo cha bilioni 59 na Serikali mkajibu mtawapa‘
‘Miaka saba baadae mkachikichia na mkwanja wa watu, Sasa leo nataka Waziri ujibu hapa, usije ukatuambia oooh! muda hautoshi. Wanajeshi wanataka kujua zile fedha zimekwenda wapi?‘
Hapa nimekusogezea hii video yake ya dakika tano kumsikiliza Halima Mdee…
ULIIKOSA HII ZAIDI YA SHILINGI TRILIONI MOJA KUTENGWA KWA AJILI YA WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA?
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE