Golikipa wa zamani wa klabu ya Simba na Yanga Juma Kaseja ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Mbeya City ya Mbeya amefunguka kuhusu goli alilofungwa na mshambuliaji wa Yanga Amissi Tambwe katika mchezo dhidi yao uliochezwa May 10 2016 katika uwanja wa Sokoine Mbeya.
“Kuhusu goli la Tambwe ni zuri najua hata yeye hakutarajia kama atafunga katika eneo kama lile ila ni goli ambalo mimi siwezi kulisahau toka nimeanza kucheza soka nilifungwa na John Baraza wakati nipo Simba na yeye akichezea Sofapaka ya Kenya lile siwezi kulisahau”
“Kuhusu mkataba na Mbeya City kwa sasa sina ulishamalizika muda tu ila nikaamua kuendelea kucheza ili kumalizia mechi za msimu zilizosalia halafu nitajua nafanyaje mwisho wa msimu, ila naomba watu wa Mbeya waisapoti timu yao na asante kwa kuwepo hapa nahisi ilikuwa mahali salama kwangu”
ALL GOALS: MBEYA CITY VS YANGA MAY 10 2016, FULL TIME 0-2
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE