Ikiwa zimepita siku 50 toka itokee ajali ya basi la Princes Muro lenye namba za usajili T 551 BQP March 25 Kimara Baruti ambapo basi lilivamia kituo kipya cha mabasi yaendayo haraka, May 11 2016 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda alielezea gharama zinazotakiwa kulipwa kwenye Kituo hicho.
Paul Makonda alizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa tayari wameshatuma bili/ gharama kwenye makampuni ambayo wanamiliki magari ya Princes Muro, ambalo limesababisha uharibifu kwenye kituo hicho……..
>>>‘kila kitu kinachofanyika hapa ni kwa ajili ya kuboresha huduma za jamii na pamoja na kuwaisha watu kufanya kazi‘
>>>’Nisingependa sisi wenyewe tuwe wa kwanza kuharibu miundombinu kuna watu tayari wanagonga barabara na kuna watu wengine wameshagonga kituo chetu maeneo ya Kimara na tayri tumempa bili ya sh. milioni 200 kwa ajili ya kukarabati kituo kile‘:– Paul Makonda
Unaweza kusikiliza hii Audio Hapa chini…
ULIIKOSA HII: USIKUTWE UMEPITA NA BODABODA KWENYE BARABARA YA MABASI YAENDAYO HARAKA DSM ITAZAME HII VIDEO HAPA CHINI…
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE