Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo.
May 25 2016 tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine, moja ya habari kubwa ni kutoka Gazeti la Jambo Leo lenye kichwa cha habari ‘Ushemeji wa Mhagama, Tanzanite One wamtia matatani Mbunge Millya’.
Gazeti hilo limeeleza kuwa tuhuma za ushemeji kati ya Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenester Mhagama na mmoja wa wabia wa Kampuni ya Sky Associates inayomiliki Mgodi wa Tanzanite One zimelisukuma Bunge kumpa siku nne Mbunge wa Simanjiro ‘CHADEMA’ James Ole Millya athibitishe madai yake kwa ushahidi.
Gazeti hilo limeieleza nukuu ya maneno ya Millya alipokuwa akitoa madai hayo alipokuwa akichangia mjadala bungeni iliyonukuliwa na Naibu Spika, Dk. Tulia ….>>> ‘Sheria za kazi zinajulikana, ni bahati mbaya kwamba Mhagama anatajwa kwamba ni shemeji wa mmoja wa wabia wa hapo. Dada anaitwa Asia Gonga ameolewa na Martin au Yusuph Mhagama’
#JamboLEO Tuhuma za Ushemeji wa Waziri Mhagama, Tanzanite One zimelisukuma bunge kumpa siku 4 Millya athibitishe pic.twitter.com/BwB9P3Aq2O
— millardayo (@millardayo) May 25, 2016
#MWANANCHI Meya K'ndoni, Boniface Jacob amebaini matumizi ya mil 392 zilizokarabati barabara hewa pic.twitter.com/fgYtCvcmDf
— millardayo (@millardayo) May 25, 2016
#MWANANCHI Muhimbili sasa yafanya upasuaji wa moyo bila mashine, upasuaji huo mkubwa ni wa kwanza kufanyika nchini pic.twitter.com/55YgmeRvpw
— millardayo (@millardayo) May 25, 2016
#MWANANCHI Kinara utengenezaji pombe bandia za kiroba, konyagi gerezani miaka 5 Moshi, miaka 7 inamsubiri Singida pic.twitter.com/86CG9QzEcM
— millardayo (@millardayo) May 25, 2016
#MTANZANIA PAC imemaliza kazi ya uchunguzi kuhusu mkataba tata kati ya Jeshi la polisi na kampuni ya Lugumi pic.twitter.com/sQScwzaBfn
— millardayo (@millardayo) May 25, 2016
#MTANZANIA Serikali imebaini maeneo matano ya ujangili ambayo pia yameingiliwa na madalali wa ndani na wa kimataifa pic.twitter.com/8rrqvcJDfJ
— millardayo (@millardayo) May 25, 2016
Mbunge Rweikiza ataka Mwigulu, Mwijage watumbuliwe kwa kuchelewa kutekeleza agizo la kupunguza tozo kwa wakulima pic.twitter.com/GPJPVDebhE
— millardayo (@millardayo) May 25, 2016
#HabariLEO Waziri Mkuu, Majaliwa amesema Tanzania ina mpango wa kujenga njia ya umeme kutoka Mbeya hadi Zambia pic.twitter.com/GJnVLfvY9W
— millardayo (@millardayo) May 25, 2016
#HabariLEO Upatikanaji sukari umeanza kuwa kwenye mwelekeo mzuri baada ya tani zaidi ya 10,000 kuingizwa kutoka nje pic.twitter.com/ZGen0SvRns
— millardayo (@millardayo) May 25, 2016
#TanzaniaDAIMA Kiwanda cha sukari cha Manyara kimeshindwa kufanya uzalishaji kutokana na ubovu wa miundombinu pic.twitter.com/kbHqrTgRDm
— millardayo (@millardayo) May 25, 2016
#JamboLEO Takukuru imeokoa bil 10 kati ya January na March ambazo zingeangukia mikononi mwa mafisadi pic.twitter.com/efWqtOrjG5
— millardayo (@millardayo) May 25, 2016
ULIIKOSA HII YA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE ILIVYOOKOA HIZI MILIONI AMBAZO ZINGETUMIKA KWA MATIBABU NJE YA NCHI ? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUB