Ni fahari kwa kila msanii sasa hivi kuona video yake imechezwa kwenye TV za kimataifa kama TRACE URBAN na MTV BASE zikiwa ni TV stations ambazo zina mamilioni ya Watazamaji kwenye nchi mbalimbali za Afrika.
Mtanzania Mayunga ambaye ni mshindi wa shindano la AIRTEL TRACE MUSIC STAR amepata shavu ya kuchezwa zaidi ya mara moja kwenye TRACE kupitia single yake mpya aliyomshirikisha Akon – ‘dont go away’
Mtanzania Vanessa Mdee ni miongoni mwa Watanzania waliochezwa pia kwenye TRACE URBAN kupitia single yake ya ‘niroge‘ na kwenye ila orodha ya nyimbo kumi kali single hii imeshika namba 4 na inaonekana imeshuka kwa nafasi kutoka wiki iliyopita lakini kwa upande wa MTV BASE ‘niroge’ imechezwa kama bonus kwenye Top10 yao.
Watanzania wengine walioshine ni Navy Kenzo na smash hit ya ‘kamatia chini‘ ambayo imeingia kwenye TOP 10 ya Africa na kushika nafasi ya nne.
Zigo remix ya Watanzania Ay featuring Diamond Platnumz imechezwa kama nafasi ya pili kwenye orodha ya video 10 kali za Afrika
Mtanzania Alikiba na smash hit ya ‘aje’ amechezwa kupitia TRACE URBAN ambapo hii ngoma yake mpya imetambulishwa kwenye time ya ngoma mpya kali zilizoachiwa na MTV BASE pia.
Nedy Music katokelezea kupitia TRACE URBAN pia, single yake mpya ya ‘usiende mbali’ aliyomshirikisha boss wake kutoka PKP Ommy Dimpoz ni moja ya ngoma zinazochezwa hata kwenye Radio na TV za Tanzania pia.
Hit single ya Ben Pol ‘moyo mashine‘ imedodoshwa kwenye kioo cha TRACE URBAN pia kama brand new video ikiwa ni video ambayo imefanywa Afrika Kusini.
HUKUONA VIDEO YA SHILOLE NA VANESSA MDEE WALIVYOKUTANA KWENYE STAGE CLUB BILLICANAS?CHEKI VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE