Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter>>>@millardayo na Zote nakusogezea hapa chini.
Moja ya story kubwa June 01 2016 kwenye gazeti la Nipashe ni yenye kichwa cha habari ‘Magufuli aishangaa Tanzania’ gazeti hilo limeripoti kuwa Rais Magufuli, amesema Tanzania ndiyo nchi pekee ambayo mwanafunzi aliyefeli kidato cha nne anaweza kujiungana chuo kikuu na kupewa mkopo na Serikali.
Gazeti hilo limesema Rais Magufuli aliyazungumza hayo wakati akikabidhi tuzo za Rais kwa mzalishaji bora wa viwanda, iliyoandaliwa na shirikisho la Viwanda Tanzania ‘CTI’
Ripoti ya Gazeti hilo imesema wiki iliyopita waziri wa elimu sayansi, teknolojia na ufundi, Prof. Joyce Ndalichako alisema kuwa ameagizwa na Rais kuwasimamisha kazi watendaji wa tume ya vyuo vikuu walihusika na na kudahili wanafunzi zaidi ya 300 wasio na sifa.
#NIPASHE JPM asema hii ndio nchi pekee mwanafunzi aliyefeli kidato cha nne anajiunga na chuo kikuu na kupewa mkopo pic.twitter.com/7nurZ7xcCb
— millardayo (@millardayo) June 1, 2016
#MAJIRA Watu wanaodhaniwa kuwa majambazi wamewaua watu wanane kwa kuwachinja na mapanga shingoni Amboni, Tanga pic.twitter.com/ku2XYBMh06
— millardayo (@millardayo) June 1, 2016
#MAJIRA Baadhi ya waliofukuzwa UDOM walazimika kutafuta vibarua ktk migahawa ili kujipatia fedha za kujikimu pic.twitter.com/gPQhJVyXT4
— millardayo (@millardayo) June 1, 2016
#NIPASHE Wabunge wa upinzani jana walisusa kushiriki kikao kilichokuwa kikiongozwa na Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson pic.twitter.com/FdNtqdeGjn
— millardayo (@millardayo) June 1, 2016
#NIPASHE Maalim Seif amehojiwa kwa saa tatu na jopo la maofisa wa idara ya upelelezi wa jeshi la polisi Zanzibar pic.twitter.com/noEJwjY0sg
— millardayo (@millardayo) June 1, 2016
#HabariLEO Wahadhiri Udom wataja kiini cha mgomo, ni kutoelewana na menejimenti ya chuo, mazingira ya ufundiahaji pic.twitter.com/zCm1beyh5k
— millardayo (@millardayo) June 1, 2016
#HabariLEO Serikali imepata majina ya wanaowauza nje ya nchi wasichana kwa kisingizio cha kuwatafutia ajira pic.twitter.com/PezZK1NsrM
— millardayo (@millardayo) June 1, 2016
#MWANANCHI Rais Magufuli ameahidi kutowaangusha wafanyabiashara wenye nia ya kuanzisha viwanda nchini pic.twitter.com/ZMcDbi2hR2
— millardayo (@millardayo) June 1, 2016
#MWANANCHI Wakati dada wa bilionea Erasto Msuya, Aneth akizikwa familia yasema inamwachia Mungu na haina hofu yeyote pic.twitter.com/tuhON4oQhL
— millardayo (@millardayo) June 1, 2016
#MTANZANIA Ukawa kuzunguka nchi nzima kuwaeleza wananchi kilichotokea bungeni hadi wabunge wa upinzani wakafukuzwa pic.twitter.com/NQPKvML0d3
— millardayo (@millardayo) June 1, 2016
#MTANZANIA Watu 1,060 wameuawa kwa wizi, wivu wa mapenzi na imani za kishirikina kati ya January na May mwaka huu pic.twitter.com/nvOe7W7GZV
— millardayo (@millardayo) June 1, 2016
#NIPASHE Mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoa ajira za moja kwa moja 1,500 na zisizo za moja kwa moja 20,000 pic.twitter.com/uGmJUgq883
— millardayo (@millardayo) June 1, 2016
#NIPASHE Katika kupambana na ajali barabarani TBS yakamata matairi 6,000 yasiyo na viwango Tanga pic.twitter.com/3iAk2QCKwD
— millardayo (@millardayo) June 1, 2016
ULIKOSA HABARI KUBWA KWENYE MAGAZETI YA JUNE 1 2016? WAHADHIRI UDOM WAONGEA, MAUAJI YA WATU 8 KWA MAPANGA TANGA, UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE