Kama utakuwa unakumbuka mnamo Mei 17, 2016 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliingia kwenye headlines baada ya kuungana na chama cha Mafundi wa magari kutoka wilaya ya Kinondoni kuyatenengeza jumla ya magari 8 ambayo yalikuwa yamekaa kwa muda mrefu ofisini kwake.
Kati ya magari nane yaliyochukuliwa na chama hicho kwaajili matengenezo mpaka sasa yaliyokamilika ni manne ambapo June 7, 2016 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alikabidhiwa rasmi.
‘Ningependa kuwaambia kwamba chama hiki cha mafundi kitakuwa ni mfano kwa mafundi wengine kwani walichokifanya kiukweli ni kitu ambacho kitaingia kwenye historia ya Tanzania kwani nisiwe muongo sijawahi sikia mafundi kama hawa waliowahi kujitolewa kwa moyo bila mimi kuwapa fedha yoyote na kuamua wenyewe kuyatengeneza magari haya‘- Paul Makonda
‘Magari manne yaliyotengenezwa watapewa watumishi ambao wamekuwa wakilalamika kuhusu usafiri pale wanapoambiwa waende kusikiliza shida za wananchi au kero za wananchi sasa sitasikia tena malalamiko’– Paul Makonda
ULIIKOSA HII YA PAUL MAKONDA KWENYE MAGARI MABOVU ALIYOYAKUTA OFISINI KWAKE ITAZAME HII VIDEO HAPA
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE