June 07 2016 zilienea taarifa kuwa Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam kumuita Kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kwa mahojiano. Zitto Kabwe amepatikana na kuthibitisha taarifa hiyo……..
>>>’Ni kweli nimepigiwa simu na mkuu wa upepelezi wa makosa ya jinai wa kanda maalum ya Dar es salaam Kamanda wambura kunifahamisha kuwa wamenihitaji leo, nimemwambia siwezi kwenda masaa yale ya saa kumi na moja ni muda wa kufuturu kwa hiyo nimemuomba niende kesho‘
Kuhusu sababu ya wito huo Zitto amesema……..>>> hilo nitalikuta polisi, polisi wana mamlaka ya kumuita raia yeyote na watampa maelezo kule kwa hiyo nitakwenda na wanasheria na baadae tutaweza kujua na nitatoa taarifa ni nini ambacho nimeitiwa’
ULIKOSA USHAURI HUU WA ZITTO KABWE KWA CCM NA CUF KUHUSU ZANZIBAR? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE