Leo June 8 2016 CCTV Africa wameripoti habari nyingine tena inayohusu ndege ya Misri iliyokuwa inatoka Cairo kuelekea Beijing China, ikiwa zimepita siku 20 toka ndege ya EgyptAir Flight 804 kuripotiwa kupoteza mawasiliano ikitokea Paris Ufaransa kuelekea Cairo, leo tena June 8 EgyptAir imegonga tena headlines.
Ndege ya EgyptAir leo June 8 iliyokuwa inatoka Cairo kuelekea Beijing China imelazimika kutua kwa dharura Uzbekistan kutokana na kuripotiwa kuwa na hofu ya bomu, maafisa wa anga wa Uzbekistan wameripoti ndege aina ya Airbus A330-220 imetua kwa dharura Uzbekistan ikiwa na abiria 118 na watumishi wa ndege 17.
Maafisa wa Misri walipigiwa simu Airport Cairo na mtu asiyejulikana na kutoa taarifa kuwa ndege hiyo aina ya Airbus A330-220 iliyokuwa inaelekea Beijing ina bomu ndani, hivyo ikabidi itue kwa dharura Uzbekistan ili kupatiwa msaada, abiria na watumishi wa ndege hiyo wameripotiwa kuwa salama.
KAMA ULIIKOSA HII YA TAKWIMU ZA AJALI ZA BARABARANI
Chanzo: CCTV Africa
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE