Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya story ambayo imeandikwa June 12 2016 kwenye gazeti la MTANZANIA ni hii yenye kichwa cha habari ‘Ujenzi kiwanja cha ndege Chato wazua nongwa’ Gazeti hilo limeripoti kuwa kusudio la Serikali kujenga kiwanja cha ndege wilaya ya Chato, Mkoa wa Geita ambako ni nyumbani kwa Rais Dk. John Magufuli limezua mjadala mkubwa.
#MTANZANIA Kusudio la Serikali kujenga kiwanja cha ndege Chato (nyumbani kwa Rais Magufuli) limezua mjadala mkubwa pic.twitter.com/HzKoqfzzRo
— millardayo (@millardayo) June 12, 2016
Gazeti hilo limesema kuwa juzi wakati mbunge wa CHADEMA David Silinde akisoma maoni ya kambi ya Upinzani bungeni, kuhusu hali ya uchumi wa Taifa, Mpango wa Maendeleo ya Taifa na Makadirio ya Mapato na matumizi ya serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017 pamoja na mambo mengine alihoji juu ya ujenzi huo.
Mtanzania limeripoti kuwa wakati akisoma maoni hayo Silinde alidai tayari uwanja huo umekwishatengewa shilingi bilioni 2 kwa ajili ya upembuzi yakinifu. Kambi hiyo ilihoji kama kuna utafiti wowote ambao Serikali imeufanya na unaonyesha kwamba ujenzi huo unamaslahi na ni kipaumbele cha Taifa kwa sasa.
Aidha Gazeti hilo limesema kuwa kambi hiyo ilishauri Serikali kwanini fedha hizo zilizokwishatengwa zisipelekwe kuimarisha viwanja vilivyopo sasa hasa ikizingatiwa kuwa serikali inataka kununua ndege tatu za shirika Ndege la ATCL.
Kauli hiyo ya Upinzani ndiyo ambayo imezua mijadala hiyo katika mitandao mbalimbali ya kijamii huku baadhi wakimnyooshea kidole moja kwa moja Rais Magufuli juu ya hatua hiyo.
Waweza kuzipitia hapa nyingine kubwa kwenye magazeti ya leo June 12 2016
#MTANZANIA Dewji ameahidi kutengeneza ajira 100,000 barani Afrika ndani ya miaka minne, watanzania kunufaika zaidi pic.twitter.com/p4yq1IolnC
— millardayo (@millardayo) June 12, 2016
#NIPASHE Waliokuwa wakipata hadi mil 40 kwa mwezi, sasa wataanza kulipwa si zaidi ya mil 15 kuanzia Julai mosi pic.twitter.com/ULTaSH1HbW
— millardayo (@millardayo) June 12, 2016
#NIPASHE Mtumishi mmoja wa zaidi ya miaka 10 Serikalini akamatwa akiwa na Shahada ya kwanza na ya uzamili, zote feki pic.twitter.com/PWb1rFPhNz
— millardayo (@millardayo) June 12, 2016
#NIPASHE Waziri Kairuki asema msimamo wa Serikali wa kuwabana watumishi kusafiri nje ya nchi bado uko palepale pic.twitter.com/baTMka7WtM
— millardayo (@millardayo) June 12, 2016
#NIPASHE Serikali kutangaza nafasi mpya za ajira za walimu mara baada ya bajeti kuu ya Serikali kupitishwa na Bunge pic.twitter.com/tH6nCog4I7
— millardayo (@millardayo) June 12, 2016
#MWANANCHI Aidai Tumbi mil 200 kwa kusababisha kifo cha mkewe mwaka 1998 Kilichotokana na uzembe wa madaktari pic.twitter.com/XthRPRFP7x
— millardayo (@millardayo) June 12, 2016
#MWANANCHI Maalim Seif amekwenda Marekani na kesho ataiambia jumuiya ya kimataifa kilichojiri uchaguzi mkuu Zanzibar pic.twitter.com/iBDAArXTaB
— millardayo (@millardayo) June 12, 2016
#JamboLEO Serikali imewataka watumishi wa umma kufanya kazi kwa bidii maarifa, weledi na kuondokana na mazoea pic.twitter.com/NGwUEzIFt2
— millardayo (@millardayo) June 12, 2016
#HabariLEO Wanafunzi shule ya msingi Mbande, Dar waunda makundi yanayolalamikiwa kuwa ndio chanzo cha kutosoma pic.twitter.com/IEGGTnAMR0
— millardayo (@millardayo) June 12, 2016
#HabariLEO Watatu wa familia moja wafariki Dodoma kwa kile kilichoelezwa ni kutokana na kula ng'ombe mwenye kimeta pic.twitter.com/p4PypX96NL
— millardayo (@millardayo) June 12, 2016
#MTANZANIA Serikali imeokoa zaidi ya bil 25.09 za watumishi hewa ktk kipindi cha miezi mitatu pic.twitter.com/JB9FFWbXhe
— millardayo (@millardayo) June 12, 2016
#TanzaniaDAIMA Masauni aagiza kukamatwa kamanda ulinzi GGM kwa tuhuma za kulazimisha wanawake kufanya ngono na mbwa pic.twitter.com/vKMvP8xXZP
— millardayo (@millardayo) June 12, 2016
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI KUTOKA AYO TV JUNE 12 2016? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE