Michuano ya Euro 2016 imeendelea tena June 17 2016 kwa michezo mitatu, ambapo mchezo mmoja tayari umeshachezwa kati ya timu ya taifa ya Italia dhidi ya timu ya taifa ya Sweden, huu ni mchezo ambao kama Sweden wangeshinda wangevunja rekodi yao ya kutoifunga Italia kwa zaidi ya miaka 15.
Katika mchezo huo ambao ulimalizika kwa Italia kuibuka ushindi wa goli 1-0, kwa goli lililofungwa na Eder Martins dakika ya 88, lakini ulikuwa ni mchezo ambao Sweden kupitia kwa nahodha wa Zlatan Ibrahuimovic alikosa nafasi ya wazi, kwa mujibu rekodi kutoka 11v11.com, Sweden mara mwisho alitoa sare na Italia June 18 2004.
Lakini kwa upande wa Sweden mara ya mwisho kupata ushindi dhidi ya Italia ilikuwa June 2 1998 katika mchezo wa kirafiki, lakini katika mchezo wa mashindano Sweden iliifunga Italia Jun 3 1987 ulikuwa mchezo wa European Championship.
Video ya goli la Italia dhidi ya Sweden
https://youtu.be/i-7SjgSjwT4
ALL GOALS: Yanga vs Al Ahly (Full Time 1-1) April 9 2016 CAF
https://youtu.be/VSM0_i0-DY0
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE