Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter>>>@millardayo na Zote nakusogezea hapa chini.
Moja ya habari iliyoripotiwa ni hii kutoka gazeti la habari leo, yenye kichwa cha habari ‘Wenye kisukari watamani uhaba wa sukari uendelee’
#HabariLEO Wenye kisukari watamani uhaba wa sukari uendelee kutokana na madhara ya sukari kwa mwili wa binadamu pic.twitter.com/7R2tj3AfKc
— millardayo (@millardayo) June 18, 2016
Gazeti hilo limeripoti kuhusu Mwenyekiti wa chama cha wenye kisukari Tanzania, Prof Andrew Swai ambaye ametamani sukari iendelee kuadimika na bei yake kuwa juu ili matumizi yake yapungue kwa jamii kutokana na madhara ya bidhaa hiyo kwa mwili wa binadamu.
Gazeti hilo limesema Prof Swai ameyazungumza hayo jana jijini Dar es salaam wakati wa semina kwa waandishi wa habari iliyolenga kuelimisha juu ya magonjwa yasiyoambukiza Prof Swai ambaye ni daktari katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alisema matumizi ya sukari ni moja ya kichocheo cha magonhjwa yasiyoambukiza kama kisukari na shinikizo la damu
Prof Swai amenukuliwa na Gazeti la Habari Leo akisema…………….>>>‘Kwa upande wa sekta ya afya tunaona ni vizuri sukari kuadimika ndio maana nchi kama uingereza inapandisha bei ya sukari kuanzia mwakani ili kudhibiti matumizi makubwa ya sukari hivyo kuongeeka bei ni njia mojawapo ya kuzuia watu wasitumie’
Hata hivyo alisema anatambua kuadimika kwa sukari nchini hakutokani na sababu za kiafya lakini ni vyema serikali kuiga hatua kama ya Uingereza na nchi zilizoendelea za kupandisha bei vitu vinavyochangia magonjwa yasiyo ambukiza kama sukari, tumbaku na vileo.
Unaweza kuzipitia hapa habari nyingine zilizoandikwa kwenye magazeti ya Tanzania
#NIPASHE Wakati Jeshi la polisi likiendelea kumtafuta Gwajima inadaiwa kuwa ametimka nchini tangu jumatano pic.twitter.com/patzcwPWqv
— millardayo (@millardayo) June 18, 2016
#NIPASHE Aliyeghushi shahada zilizomwezesha kupata wadhifa mkubwa alioutumikia zaidi ya miaka 10 sasa anachunguzwa pic.twitter.com/0Oqvo6pwBB
— millardayo (@millardayo) June 18, 2016
#MTANZANIA Wabunge CHADEMA, Suzan Lyimo na Anatropia Theonist wasimamishwa kuhudhuria vikao kwa kosa la kusema uongo pic.twitter.com/G6DGl4NzGU
— millardayo (@millardayo) June 18, 2016
#MTANZANIA Wanazuoni watofautiana kuhusu mwenendo wa uongozi na hatua za kinidhamu zinazochukuliwa na Rais Magufuli pic.twitter.com/DVuiHpfJoF
— millardayo (@millardayo) June 18, 2016
#MTANZANIA TCRA imezima namba tambulishi (IMEI) 603,000 sawa na 2.9% ya vifaa vya mawasiliano pamoja na simu feki pic.twitter.com/ZnpeL7hpJj
— millardayo (@millardayo) June 18, 2016
#MTANZANIA Mahakama Dar imewahukumu wanane faini 400,000 baada ya kupatikana na hatia ya kuombaomba na uzururaji pic.twitter.com/oP7XffKVJa
— millardayo (@millardayo) June 18, 2016
#HabariLEO Waziri Simbachawene amemuagiza RC Makonda kuhakikisha hakuna mfanyabiashara ktk maeneo ya 'mataa' pic.twitter.com/w1rckQ8O0V
— millardayo (@millardayo) June 18, 2016
#HabariLEO Benki ya dunia imetoa nyongeza ya fedha bilioni 400 kwa ajili ya miradi ya kuondoa umaskini pic.twitter.com/cOJNiv4fCw
— millardayo (@millardayo) June 18, 2016
#HabariLEO Anusurika kuuawa kwa mapanga baada ya bibi yake kumuuza kwa wauaji ili wachukua sehemu ya viungo vyake pic.twitter.com/zMVozDf73H
— millardayo (@millardayo) June 18, 2016
#MWANANCHI RC Makonda amesema bodaboda wasiovaa helmet watakamatwa na kushtakiwa kwa kosa la kutaka kujiua pic.twitter.com/lof98hE10U
— millardayo (@millardayo) June 18, 2016
#MWANANCHI Waziri Mwijage akiri tatizo la sukari hata yeye linamsumbua kutokana na shida wanayopata Watanzania pic.twitter.com/SAhrWlhQZQ
— millardayo (@millardayo) June 18, 2016
#MWANANCHI Utafiti umeonyesha 92.6% wenye shinikizo la damu nchini hawafahamu kama wanaugua ugonjwa huo pic.twitter.com/aPvyKdIowo
— millardayo (@millardayo) June 18, 2016
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI JUNE 18 2016 KUTOKA AYO TV UNAWEZA KUAN GALIA VIDEO HII HAPA CHINI?
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE