Siku kadhaa zilizopita kijiji cha Sanya Hoye kilipitisha adhabu ya faini ya Shilingi 50,000 pamoja na viboko 15 kwa atakayekutwa baa na mtoto mdogo au kuvaa nguo fupi. Adhabu hiyo imeanza kutekelezwa ambapo juzi wameshachapwa wanawake wawili Kwa kukiuka sheria hiyo.
Mme wa miongoni mwa wanawake waliochapwa Ali Maulid Njiwa amesema……>>>’Nashukuru sana mwenyekiti mke wangu alichapwa, alikuwa akifanya hivyo kwa muda mrefu na amekuwa akiambiwa hasikii kwa hiyo walikamatwa na kuchapwa viboko 15′
Kingine kutoka kwenye kijiji hicho ni kwamba watakaotumia fedha za mradi wa TASAF visivyo wamekubaliana watawaadhibiwa Kwa viboko 10, Mwenyekiti wa kijiji cha Sanya Hoye, Moses Mnuo ametoa ufafanuzi wa maazimio hayo katika kikao cha kijiji cha Sanya Hoye………
>>>’baada ya kugundulika kwamba kuna baadhi wanatumia fedha tofauti na utaratibu, tukakaa na wenye mradi tukafikia maazimio kwamba watachapwa fimbo 10 na kupewa elimu na wakiendelea tutawaondoa kwenye mradi’
Unaweza kuangalia hii video kwa kubonyeza play hapa chini
ULIKOSA HII MARUFUKU YA KUTEMBEA NA MTOTO SANYA OYE USIKU? BONYEZA PLAY HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER