Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imechukua hatua mbalimbali katika kulinda na kuimarisha haki za binadamu kwa kuridhia mikataba mbalimbali ya haki za binadamu ya kimataifa na kikanda, kufuta sheria zinazokinzana na katiba na haki za binadamu na kuanzisha Tume ya haki za binadamu na utawala bora.
Akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa majukumu ya ofisi ya mwanasheria mkuu wa Serikali, Kaimu Mkurugenzi wa divisheni ya katiba na haki za binadamu ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, Alesha Nguya amesema Tanzania imekuwa nchi ya kwanza Afrika Mashariki kwa kuwa na mpango kazi wa haki za binadamu ambao baadhi ya nchi zimeiga mpango huo.
Licha ya kufanya vizuri imepewa mapendekezo 227 na yaliyokubaliwa ni 130 ambayo hayakinzani na katiba na sera za nchi na 72 yalikataliwa kwa sababu hayaendani na mfumo wa kisheria, sera, imani za dini na utamaduni na desturi. (mapendekezo hayo yanahusu kufutwa kwa adhabu ya kifo, masuala ya ubakaji ndani ya ndoa na mapenzi ya jinsia moja.
ULIKOSA HII YA BUNGE KUTAKA KUJADILI KITENDO CHA ALIYEMTUKANA RAIS MAGUFULI KUCHANGIWA FEDHA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB INSTAGRAM YOUTUBE