Mmiliki wa klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Moise Katumbi amehukumiwa kwenda jela, Katumbi ambaye ni boss wa TP Mazembe ambayo ilikuwa inachezewa na nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu.
Katumbi amehukumiwa miaka mitatu sambamba na kutozwa faini ya dola milioni 6 kwa kosa la kujimilikisha eneo, Katumbi pia alikuwa anatajwa kugombea nafasi ya Urais wa Kongo mwishoni mwa mwaka 2016 kupitia chama cha upinzania kushinda na Rais anayemaliza muda wake Joseph Kabila.
Hata hivyo wakati wa kutolewa hukumu hiyo Moise Katumbi hakuwepo Kongo, siku moja kabla ya hukumu alikuwa kasafiri kwenda Afrika Kusini kupata matibabu, makosa mengina anayotuhumiwa nayo Katumbi ni pamoja na kutajwa kuajiri wa geni kutoka nje ya Kongo kwa ajili ya kuandaa njama za kumuondoa Rais Kabila.
Moise Katumbi ndio Rais wa klabu ya TP Mazembe aliyoingoza kucheza hadi hatua ya fainali ya klabu Bingwa ya dunia dhidi ya Inter Milan December 18 2010, rekodi ambayo hakuna klabu ya Afrika imewahi kuifikia, TP Mazembe ndio ya kwanza, TP Mazembe wanakuja Tanzania June 28 kucheza mchezo wao wa pili wa nane bora dhidi ya Yanga.
GOAL AND HIGHLIGHTS: MO BEJAIA VS YANGA JUNE 20 2016, FULL TIME 1-0
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE