Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya stori iliyoripotiwa ni hii kwenye gazeti la Nipashe yenye kichwa cha habari ‘Maumivu 18% miamala benki ’
#NIPASHE Takribani benki zote nchini zimetangaza ongezeko la 18% kwenye huduma za kuhifadhi na kutoa fedha pic.twitter.com/64uHOC31YY
— millardayo (@millardayo) July 1, 2016
Baada ya taribani benki zote nchini kutangaza ongezeko la asilimia 18 kwenye huduma za kuhifadhi na kutoa fedha, kupitia gazeti la Nipashe wachumi mbalimbali walisema jana kuwa mbali na wafanyakazi ambao wataathirika na ongezeko hilo kwa sababu ya mishahara yao inapitia benki wamo wafanyabiashara na wanafunzi.
Gazeti hilo limeripoti kuwa wafanyabiashara, wanafunzi na wengine wote wanaotumia huduma za kibenki wataumia pia kwa kukatwa fedha zaidi wanapofanya miamala ya kibenki, walisema hali hiyo inaweza kufanya watu waamue kukaa na fedha majumbani mwao kitendo ambacho kitaongeza matukio ya uhaifu kwa majambazi kuvamia majumabani.
Gazeti hilo limesema kuwa Ongezeko hilo limetokana na marekebisho ya sheria ya kodi ya ongezeko ya thamani ‘VAT’, SURA 148, yaliyotangazwa na Waziri wa fedha na mipango, Dk Philip Mpango alipokuwa akisoma bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Mpango alisema Serikali inakusudia kutoza kodi ya ongezeko la thamani kwenye ada za huduma za kibenki zinazotozwa na benki zote nchini ili kupanua wigo wa kodi.
Unaweza kuzipitia hapa habari nyingine kubwa kwenye magazeti ya leo julai mosi
#NIPASHE TAKUKURU yamtaja kinara wa wizi mil 7 kila dakika kuwa ni Mohamed Murtaza Yusuph Ali pic.twitter.com/P0LkFxMvMH
— millardayo (@millardayo) July 1, 2016
#NIPASHE Waziri Mkuu, Majaliwa amewataka wabunge wa upinzani kurudi bungeni ili washirikiane kuishauri Serikali pic.twitter.com/z15Y34aOod
— millardayo (@millardayo) July 1, 2016
#NIPASHE Tundu Lissu apata dhamana huku wafuasi wake wakikamatwa na kushikiliwa na jeshi la polisi pic.twitter.com/eRRYG4iSVs
— millardayo (@millardayo) July 1, 2016
#MWANANCHI Utekelezaji Sheria ya fedha kuanza leo ambapo VAT itatozwa huduma za mitandao ya simu na taasisi za fedha pic.twitter.com/roFMH2dHxl
— millardayo (@millardayo) July 1, 2016
#MWANANCHI Jela miaka 60 kwa kumlawiti mkewe mjamzito, alifanya kitendo hicho siku 3 mfululizo na kumuathiri kiafya pic.twitter.com/fPiuKmwO98
— millardayo (@millardayo) July 1, 2016
#JamboLEO UKAWA wavaa nguo nyeusi na kubeba mabango yenye ujumbe mbalimbali wa shutuma dhidi ya Rais Magufuli pic.twitter.com/MiG13tibkM
— millardayo (@millardayo) July 1, 2016
#JamboLEO Makaburi mawili ya watoto wachanga yamefukuliwa na miili yao kuchukuliwa na watu wasiojulikana Geita pic.twitter.com/CK0vqDb5te
— millardayo (@millardayo) July 1, 2016
#MTANZANIA Mtoto Nurad darasa la nne shule ya msingi bunge aliyetinga kwa msajili kuanzisha chama chake cha siasa pic.twitter.com/OAt0yAZEcT
— millardayo (@millardayo) July 1, 2016
#HabariLEO Mahakama maalumu ya kushughulikia makosa ya rushwa na ufisadi, inaanza rasmi leo Julai Mosi pic.twitter.com/fnvnVpu2Sr
— millardayo (@millardayo) July 1, 2016
#HabariLEO Serikali yataka DPP kuchukua hatua stahiki kesi ya aliyemtukana JPM mtandaoni, aliyeadhibiwa kulipa faini pic.twitter.com/GLyR2nUktW
— millardayo (@millardayo) July 1, 2016
#MWANANCHI Naibu waziri wa ajira, Mavunde amesema kiwango cha chini cha mshahara bado ni 100,000 kwa mwezi pic.twitter.com/YIWPT4KHL0
— millardayo (@millardayo) July 1, 2016
#NIPASHE Serikali itaanzisha kikosi maalum cha kufuatilia kwa karibu matumizi ya mashine za kielektroniki 'EFD' pic.twitter.com/doeEIslWxG
— millardayo (@millardayo) July 1, 2016
#NIPASHE Mwanasayansi na Mwalimu UDSM, Donath Damian amesema matumizi ya mtindi ni tiba sahihi ya ugonjwa wa fangasi pic.twitter.com/svNhlvRJ6O
— millardayo (@millardayo) July 1, 2016
#MWANANCHI Kuenguliwa kwa DC dakika za lala salama kwaibua maswali mengi kuliko majibu pic.twitter.com/1bEX2UG8VE
— millardayo (@millardayo) July 1, 2016
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI JULY 01 2016 KUTOKA AYO TV? UNAWEZA KUTAZAMA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE