Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya stori iliyoripotiwa ni hii kwenye gazeti la Habari Leo yenye kichwa cha habari ‘Mwarobaini wizi wa bodaboda wapatikana’
#HabariLEO VETA imebuni kifaa cha kudhibiti wizi wa magari na pikipiki za abiria kwa kutumia simu pic.twitter.com/9VN9tJMJWj
— millardayo (@millardayo) July 3, 2016
Gazeti hilo limeripoti kuwa mamlaka ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi ‘VETA’ imebuni kifaa cha kudhibiti wizi wa magari na pikipiki za abiria maarufu bodaboda kwa kutumia simu ambapo kwa kutumia kifaa hicho, dereva atakuwa na uwezo wa kuzima pikipiki au gari kwa kutumia simu ya mkononi ambayo namba yake itakuwa imefungwa katika chombo hicho.
Akizungumzia kuhusu kifaa hicho Mwalimu wa Teknolojia ya mwasilliano wa VETA , Valerian Sanga alisema alishirikiana na mwalimu mwenzake wa chuo hicho anayefundisha masuala ya umeme, Christian Brighton kubuni kifaa hicho kilichowachukua miaka miwili.
Sanga alisema kifaa hicho kina GPS na kinatumia mawasiliano ya simu kwa kutumia GSM itakayosaidia kujua sehemu pikipiki au gari lilipo, lakini pia kikimwezesha mmiliki kuzima na kuwasha usafiri wake popote ulipo pia sasa wanafunga kifaa hicho kwa gharama ya sh 400,000 lakini wanatarajia baadaye watakapopata oda nyingi, watapunguza bei.
Unaweza kuzipitia hapa chini habari nyingine kubwa kwenye magazeti ya July 03 2016
#MWANANCHI Makonda atangaza vita nyingine, hataki uvutaji shisha asema inachanganywa na vilevi vinavyoharibu vijana pic.twitter.com/K3xyM5BBJ9
— millardayo (@millardayo) July 3, 2016
#MWANANCHI CAG asema halmashauri 34 zimetumia trilioni 1.45 kugharimia shughuli ambazo hazikuwamo kwenye bajeti pic.twitter.com/E7MmR1wDOJ
— millardayo (@millardayo) July 3, 2016
#MWANANCHI Mawakili 30 matatani kwa kukiuka maadili ikiwamo kung'ang'ania majalada ya kesi za wateja pic.twitter.com/6OUGJ8QUW6
— millardayo (@millardayo) July 3, 2016
#JamboLEO Rais Magufuli awapa majukumu mazito baadhi ya askari wa JWTZ kwa kuwateua kushika nafasi kadhaa nyeti pic.twitter.com/m5QHRzbB1o
— millardayo (@millardayo) July 3, 2016
#TanzaniaDAIMA Tafiti WHO; watoto 143,000 hufa kutokana na madini ya risasi kwenye rangi za mafuta za kupamba nyumba pic.twitter.com/iohCGgsrge
— millardayo (@millardayo) July 3, 2016
#TanzaniaDAIMA SMZ yapiga marufuku bastola bandia za watoto kutokana na athari mbaya wazipatazo watoto pic.twitter.com/TbZ2OWuzGE
— millardayo (@millardayo) July 3, 2016
#TanzaniaDAIMA Aliyedaiwa kuiibia Serikali kwa EFDs adaiwa kutoroka, polisi wasema taarifa hizo hazina ukweli pic.twitter.com/F3y07ww0xK
— millardayo (@millardayo) July 3, 2016
#MWANANCHI Aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Ally Muswanya ameachia wadhifa huo hata kabla ya kuapishwa pic.twitter.com/OxB9kso0ai
— millardayo (@millardayo) July 3, 2016
#MWANANCHI Baada ya TCRA kuzima simu bandia baadhi ya mafundi wa simu Mwanza walia njaa kwa madai hawapati wateja pic.twitter.com/uosMi9rMo2
— millardayo (@millardayo) July 3, 2016
#NIPASHE Serikali yaombwa kufuta kodi mafuta ya albino kwa kuyatoa kwenye kundi la vipodozi na kuweka kwenye dawa pic.twitter.com/ClzXV7fhXW
— millardayo (@millardayo) July 3, 2016
#MWANANCHI Kocha wa Yanga, Pluijm asema wanafungwa kutokana na kukosa uzoefu mechi za kimataifa, maarifa ya mchezo pic.twitter.com/m9rC2Lm2i5
— millardayo (@millardayo) July 3, 2016
#LeteRAHA Baada ya kuingia mkataba na Kocha Omog sasa Simba imehamia kwenye usajili wachezaji bora wa kigeni pic.twitter.com/g89EvfYCcX
— millardayo (@millardayo) July 3, 2016
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI JULY 03 2016 KUTOKA AYO TV? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI