Taarifa niliyoipokea kutoka ikulu jijini Dar es salaam ni kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Leonard Lutegama Maboko kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS).
Taarifa hiyo ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi huu umeanza July 07 2016. Kabla ya uteuzi huu Dkt. Leonard Lutegama Maboko alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya binadamu Mbeya (NIMR Mbeya).
Dkt. Leonard Lutegama Maboko anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Fatma Mrisho ambaye mkataba wake umemalizika tangu June 30 2016.
JPM amemteua Dk. Leonard Lutegama Maboko kuwa Mkurugenzi Mtendaji TACAIDS, anachukua nafasi ya Dk. Fatma Mrisho ambaye mkataba umemalizika
— millardayo (@millardayo) July 8, 2016
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI KUTOKA AYO TV JULY 08 2016? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI