Baada ya Rais Magufuli kutangaza elimu bure kuanzia elimu ya msingi mpaka kufikia kidato cha nne, kumekuwa na changamoto kubwa ya uhaba wa madawati ambapo Serikali ilianzisha kampeni ya uchangiaji wa madawati.
Sasa leo July 14, 2016 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amepokea milioni 27 kutoka ofisi ya Mbunge Mussa Azzan Zungu jimbo la Ilala
‘Elimu ndani yake kuna walimu, ndani yake kuna maabara, ndani yake kuna madawati, ndani yake kuna madarasa, ndani yake kuna vitu kwahiyo mtu akisema Elimu ni kitu kikubwa ambacho kina mambo tofauti tofauti na ndio maana Rais wetu ameanza kutoa Elimu bure’- RC Paul Makonda
ULIIKOSA HII YA CRDB KUKABITHI MILIONI 100 KWA PAUL MAKONDA BASI ITAZAME HII VIDEO HAPA