Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya yalioandikwa ni huu utafiti wenye kwenye gazeti la Mtanzania yenye kichwa ‘Uhusiano wa kula matunda na furaha’
#MTANZANIA Utafiti: Ulaji wa matunda na mboga za majani unaweza kukusaidia kupata furaha pic.twitter.com/poXGW0EKzJ
— millardayo (@millardayo) July 18, 2016
Ulaji wa matunda na mboga za majani unaweza kukusaidia kupata furaha, utafiti mmoja wa Australia umegundua. Watafiti hao wamegundua kuwa watu waliobadili mtindo wao wa ulaji, na kuanza kula matunda na mboga za majani kwa wingi katika mlo wao wa kila siku wamepatwa na ongezeko la kuwa na hisia za furaha na kuridhikaa kimaisha ikilinganishwa na namna ile ile ambayo mtu asiye na ajira anavyohisi mara apatapo ajira limeeleza jarida ‘la American Journal of Public Health.
Redzo Mujcic ambaye ni mtafiti mwenza wa afya na uchumi katika chuo kikuu cha Queensland nchini Australia amesema……..>>>”Ni wazi kuwa ulaji wa matunda na mboga za majani huongeza furaha yetu kwa kasi zaidi kuliko inavyoongezeka kutokana na afya ya muhusika’‘
Utafiti uliofanyika kabla ya huo ulionyesha kwamba kula mboga na matunda mengi kumesaidia mno kuimarisha sana afya ya miili ya watu, lakini faida kama hizo zinaanza kuonekana baada ya kipindi kirefu cha wakati, wamesema watafiti hao.
Unaweza kuzipitia hapa habari nyingine kubwa zilizoandikwa kwenye magazeti y leo July 18 2016
#MWANANCHI Ajali ya lori yaua watatu Bahi na kujeruhi 19, dereva wa lori alitoroka baada ya ajali hiyo pic.twitter.com/5XXaMRe1yF
— millardayo (@millardayo) July 18, 2016
#MWANANCHI Kiwanda cha Royal Soap chatozwa faini mil 10 kwa kutiririsha maji yenye sumu kwenye makazi ya watu pic.twitter.com/UlCuUa4iZ3
— millardayo (@millardayo) July 18, 2016
#MWANANCHI CCM Arusha yajipanga kumtimua Mwenyekiti wake Longido kwausaliti na kutoshiriki shughuli mbalimbali pic.twitter.com/EY9npVlP0Q
— millardayo (@millardayo) July 18, 2016
#NIPASHE Malecela afunguka JPM kupewa chama, asema azingatie kutoa nafasi zaidi kwa vijana ktk safu atakayounda pic.twitter.com/9TZqNICXEU
— millardayo (@millardayo) July 18, 2016
#NIPASHE Makinda amesema mabadiliko ya uongozi ndani ya NHIF yanalenga kuimarisha utekelezaji na uwajibikaji pic.twitter.com/qudlIDPYSN
— millardayo (@millardayo) July 18, 2016
#NIPASHE TBS imekifungia kiwanda bubu Dar kilichokuwa kinachakata vilainishi vya mashine kwa zaidi ya miaka 30 pic.twitter.com/SQaRFgPMmV
— millardayo (@millardayo) July 18, 2016
#NIPASHE Awamu ya pili ya ujenzi wa barabara za mabasi ya haraka unatarajiwa kutoka Dar hadi Vikindu mkoani Pwani pic.twitter.com/9SbjSpaCqO
— millardayo (@millardayo) July 18, 2016
#NIPASHE Mil 71 za wanachama CHF Igunga, Tabora zinadaiwa kupotea ktk mazingira ya kutatanisha pic.twitter.com/gpVaJQiwBu
— millardayo (@millardayo) July 18, 2016
#NIPASHE Marekani imeionya Uturuki dhidi ya "kutuhumu hadharani' kuwa ilihusika ktk mapinduzi yaliyoshindwa pic.twitter.com/5zi6wzKy3a

#JamboLEO Waziri Mkuu Majaliwa apiga marufuku matumizi ya viberiti, mishumaa, hita za kuchemshia maji shule za bweni pic.twitter.com/5RIzUThrJ2
— millardayo (@millardayo) July 18, 2016
#JamboLEO Vitendo vya ubakaji, ulawiti kwa watoto kati ya miaka mitano na 15 vimeongezeka na kufikia 19 kila siku pic.twitter.com/nzkr0LHyj7
— millardayo (@millardayo) July 18, 2016
#JamboLEO Limebaini kuwepo kwa kambi ya mafunzo ya vitendo vya uhalifu ndani ya mapango ya Amboni kwa zaidi miaka 15 pic.twitter.com/ceBDkFKOwQ
— millardayo (@millardayo) July 18, 2016
#MAJIRA JUVICUF wataka ufafanuzi NEC kuhusu baadhi ya makada CCM kuteuliwa nafasi mbalimbali za uongozi serikalini pic.twitter.com/IrRyDzco5j
— millardayo (@millardayo) July 18, 2016
#TanzaniaDAIMA IGP Mangu amesema muda wowote wanaweza kumfikisha mahakamani Maalim Seif kwa tuhuma za uchochezi pic.twitter.com/wDfwqpI9Us
— millardayo (@millardayo) July 18, 2016
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI JULY 18 2016 KUTOKA AYO TV? UNAWEZA KUIANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI