Baada ya Jeshi la polisi kupiga marufuku mikutano hadhara na maandamano ya kisiasa, leo July 21 2016 Chama cha demokrasia na maendeleo ‘CHADEMA’ kimefungua kesi katika mahakama ya Afrika Mashariki dhidi ya serikali kuhusu kuzuiliwa kufanya mikutano hiyo hapa nchini.
Naibu katibu mkuu CHADEMA bara, John Mnyika amesema wamefikia uamuzi huo kutokana na ukiukwaji wa ibara ya 6 na 7 ya mkataba wa uanzishwaji wa Jumuiya Afrika Mashiriki……..
>>>Inaletwa mahakamani kwa kukiuka mkataba wa afrika mashariki ibara ya 6 na 7 ya, tumeleta vielelezo vya barua yenyewe ya zuio la polisi kama ushahidi wa kwamba kweli polisi wa Tanzania wametoa agizo kama hili, tumeleta vielelezo vya mikutano ambayo imezuiwa, mikutano ya Kahama, mahafali ya wanachuo wa CHADEMA kule Dodoma, mahafali yaliyofanyika Moshi‘
ULIKOSA HII YA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI KUKUTANA KWA DHARURA? UNAWEZA KUNAGALIA VIDEO HII HAPA CHINI