Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya yalioandikwa ni huu utafiti wenye kwenye gazeti la Jambo leo yenye kichwa ‘TCU: Hakuna vyuo vilivyofungiwa ”
#JamboLEO TCU yakanusha taarifa za kuvifungia udahili wa kozi tofauti vyuo 22 zilizozagaa juzi pic.twitter.com/3AS6MUsqcC
— millardayo (@millardayo) July 26, 2016
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imewatoa hofu wanafunzi waliohitimu katika vyuo vilivyozuiwa hivi karibuni kufanya udahili, huku ikikanusha taarifa za kuzifungia udahili wa kozi tofauti vyuo 22 zilizozagaa juzi.
Hivi karibuni TCU ilitangaza kusimamisha kufanya udahili vyuo vitano baadhi vikiwamo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo Kikuu cha Mtakatifu Francis cha Ifakara Morogoro, Chuo cha Mtakatifu Joseph cha Dar es Salaam na Chuo cha IMTU cha Dar es Salaam vyote kwa kozi ya udaktari.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana, Kaimu Katibu Mtendaji wa TCU, Eliuther Mwageni alisema kufungiwa kwa vyuo hivyo ni kwa muda mpaka vitakapokabidhi vigezo vinavyotakiwa.
Mwageni alisema…….>>>”Kuna vigezo vinavyotakiwa kufikiwa ili chuo kiweze kusajiliwa na hivi vyuo hatujavifungia ila tumevisimamisha kwa muda mpaka vikidhi vigezo vyetu.
Kuhusu taarifa za vyuo 22 kusimamishwa kudahili wanafunzi katika kozi mbalimbali zilizozagaa kwenye mitandao juzi na jana, Mwageni alisema……>>> ‘taarifa hizo ni za uzushi, zina lengo baya hivyo hazina ukweli wowote‘.
Source: Gazeti la Jambo Leo
#JamboLEO Hillary Clinton amewaalika Maalim Seif na Zitto Kabwe kuhudhuria kongamano maalumu la chama cha Democratic pic.twitter.com/vecsHg3FD7
— millardayo (@millardayo) July 26, 2016
#NIPASHE SUMATRA kumfikisha mahakamani mkurugenzi mtendaji UDART kwa kosa la kutoza nauli kinyume na bei elekezi pic.twitter.com/hEo29JS6Cn
— millardayo (@millardayo) July 26, 2016
#MWANANCHI Waziri mkuu, Kassim Majaliwa amejipa mwezi mmoja kuhamia Dodoma pic.twitter.com/63MNMW6a5v
— millardayo (@millardayo) July 26, 2016
#MWANANCHI Mzee wa upako amesema kitendo cha viongozi CCM kutaja zaidi jina la Lowassa ni ishara kuwa yeye ni tishio pic.twitter.com/rTJlJjBoOw
— millardayo (@millardayo) July 26, 2016
#MWANANCHI Mshtakiwa wa mil 7 kwa dakika kupandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka mengine ya uhujumu uchumi pic.twitter.com/nHMb4ukGpQ
— millardayo (@millardayo) July 26, 2016
#MWANANCHI Mbunge wa Karatu na wa viti maalumu Arusha wote CHADEMA kuhojiwa kutokana na kufanya mikutano ya hadhara pic.twitter.com/Heo6yeMVdS
— millardayo (@millardayo) July 26, 2016
#MWANANCHI Koffi Olomide ameomba radhi mashabiki kwa kitendo cha kumpiga mnenguaji wa kundi lake. pic.twitter.com/5e5rhrNjBU
— millardayo (@millardayo) July 26, 2016
#NIPASHE Waandishi wa habari 42 Uturuki kukamatwa kama sehemu ya upelelezi wa jaribio la mapinduzi July 15 pic.twitter.com/pTVJbirN71
— millardayo (@millardayo) July 26, 2016
#TanzaniaDAIMA Makongoro Nyerere anusurika ajalini akitokea kwenye mkutano mkuu wa CCM pic.twitter.com/fP3mT7CCZp
— millardayo (@millardayo) July 26, 2016
#MTANZANIA JKCI inatarajia kufanya kipimo cha mwisho kabla ya kumruhusu mtoto aliyewekewa betri kwenye moyo wake pic.twitter.com/kakIG3487O
— millardayo (@millardayo) July 26, 2016
#MTANZANIA Abiria UDART walalamika kukaa muda mrefu vituoni kutokana na kusuasua mtandao wa tiketi tofauti na kadi pic.twitter.com/iw2MplMvFV
— millardayo (@millardayo) July 26, 2016
#MTANZANIA Mkurugenzi Mwanza awafungia nje dakika 30 watumishi wa halmashauri hiyo waliochelewa kuripoti kazini pic.twitter.com/RG4G2g8kkR
— millardayo (@millardayo) July 26, 2016
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI JULY 26 KUTOKA AYO TV UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI