Mtandao maarufu wa Daily Mail umetaja orodha ya majengo ambayo yana thamani kubwa zaidi duniani, orodha hiyo iliyochapishwa kwenye mtandao huo July 26 2016 imetaja majengo hayo pamoja na gharama zake.
1. Masjid al -Haram jengo lipo Mecca, Saudia Arabia na lina thamani ya kushangaza ambapo inatajwa kuwa ni dola bilioni 100 na limekuwa nafasi ya juu katika orodha ya majengo ya gharama kubwa zaidi duniani. Jengo hili lilianza kujengwa mwaka 638 na linatarajiwa kukamilika 2020
2. ABRAJ AL NAIT, jengo hili liko nchini Saudi Arabia na gharama yake ni Dola bilioni 15 lilijengwa 2012
3. Resorts World Sentosa lipo Singapore na thamani yake ni Dola bilioni 6.59, lilijengwa 2012
4. Marina Bay Sands lipo Singapore ni la nne katika orodha, na lina thamani ya dola bilioni 5.5, lilijengwa 2010
5. The Cosmopolitan lipo Marekani na thamani yake ni dola bilioni 3.90, lilijengwa 2010
6. One World Trade Center lipo New York Marekani na lina thamani ya Dola Bilioni 3.8, lilijengwa 2012
7. Emirates Palace lipo Abu Dhabi, United Arab Emirate lina thamani ya Dola Bilioni 3 na ni jengo la hoteli la pili ambalo ni ghali zaidi duniani, lilijengwa 2005
8. Wynn Resort, inajulikana kama moja ya hoteli nzuri zaidi duniani na jengo lina thamani ya Dola bilioni 2.7 lipo Marekani, lilijengwa 2005
9. City of Dreams lilijengwa mwaka 2009 lipo Macau, China na thamani yake ni dola bilioni 2.4
10. The Venetian Macao lilijengwa mwaka 2005 Macau, China na liligharimu dola bilioni 2.4
11. The Princess Tower, ni jengo la pili kwa urefu Dubai na lilipata kuwa jengo refu duniani kwa makazi lakini nafasi ikawa imechukuliwa na 432 Park avenue la New York, lilijengwa 2012 na thamani yake ni dola bilioni 2.17
12. Jengo la Antilla lipo Mumbai, India ni jengo linalomilikiwa na mtu binafsi anaitwa Mukesh Ambani, thamani yake ni dola bilioni 2, lilijengwa 2010
13 The Palazzo lipo United States na gharama yake ni dola bilioni 1.8, lilijengwa 2007
14. Taipei 101 lipo Taiwan na lina thamani ya Dola bilioni 1.8, lilijengwa 2004
15 Bellagio lilijengwa mwaka 1998 na lina thamani ya dola bilioni 1.6, lipo USA
16. Seat of the ECB ni Jengo la Makao ya Benki Kuu ya Ulaya lilijengwa mwaka 2013 Frankfurt, Germany na lina thamani ya dola bilioni 1.57.
17. Wembley Stadium una vyoo 2,618, uwanja upo London na ni uwanja wa pili kwa ukubwa Ulaya na thamani yake ni dola bilioni 1.5, ulijengwa 2006
18. Yankee Stadium ulijengwa 2009, uwanja huu una thamani ya dola bilioni 1.5 upo New York Marekani
19. Burj Khlaifa, lilijengwa 2010 lipo Dubai, inaelezwa kuwa kama madirisha yake yangekuwa yanasafishwa kawaida ingehitaji wafanyakazi 36 miezi minne kusafisha jengo, thamani yake ni dola bilioni 1.5
20. Petronas Twin Tower, jengo hili lipo Kuala lumpur, Malaysia na lilijengwa mwaka 1999 na lina thamani ya dola bilioni 1.16
ULIKOSA HII YA BILIONEA MTANZANIA KATOA SABABU ZA KWANINI HAJANUNU NDEGE BINAFSI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
VIDEO