July 28 2016, Mahakama kuu kanda ya Tanga ilitangaza maamuzi rasmi ya kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge iliyokuwa ikimkabili Mbunge wa Pangani Jumaa Aweso wa Chama cha mapinduzi (CCM) iliyofunguliwa na mbunge wa chama cha wananchi(CUF) Amina Mwidau
Ayo TV imefanya exclusive interview na Mbunge Jumaa Aweso ambaye anatueleza hatua atayochukua baada ya kushinda keshi hiyo ikiwa ni pamoja na kulipwa milioni 60 kama gharama za usumbufu.
‘Uchaguzi kuna kushinda na kushindwa, baada ya kushinda mpinzania wangu hakuridhika na matokeo na akasema kwamba wafuasi wangu walimkejeli kwa kumuita Bi. kidude lakini pia yeye ni mwanamke asiyefaa kauli ambazo hazikutolewa‘ –Jumaa Aweso
‘Mahakama kuu ya Tanga ikatoa taarifa kwamba hakukuwa na uthibitisho wowote wa kimsingi na kunitangaza mimi kuwa mbunge halali wa jimbo la Pangani‘ –Jumaa Aweso
Kiasi gani cha gharama amepoteza tangu kesi hiyo imeanza kusikilizwa mahakamani? Jumaa Aweso amefunguka…>>>’Kesi hii imedumu kwa takribani miezi tisa na imegharimu takribani milioni 60 na nilazima azilipe zikasaidie kutatua matatizo ya Pangani‘
Unaweza kuendelea kumsikiliza kwenye hii audio hapa chini….
ULIIKOSA HII YA MBUNGE JUMAA AWESO KUHUSU TATIZO LA MAJI PANGANI