Mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast aliyekuwa anaichezea klabu ya Azam FC Kipre Tchetche sasa ni rasmi hatoichezea tena klabu ya Azam FC katika msimu mpya unaotarajia kuanza hivi karibuni.
Awali mshambuliaji huyo aliripotiwa kwenda kujiunga na klabu za Uarabuni na kuachana na Azam FC, kitu ambacho viongozi wa Azam FC walikanusha na kusema kuwa wana mkataba na mchezaji huyo.
Kwa sasa naweza kusema ni rasmi staa huyo hatokuwa tena na Azam FC, hiyo inatokana na yeye kutambulishwa rasmi katika klabu ya Al Nahdha ya Oman na kupewa jezi namba 10.
Aliyekuwa mshambuliaji wa Azam FC Kipre Tchetche amekabidhiwa jezi namba 10 katika timu yake mpya ya Al Nahdha. pic.twitter.com/MqV8v7FJTL
— millard ayo (@millardayo) August 4, 2016
ALL GOALS: SIMBA VS COASTAL UNION FA CUP APRIL 11 2016, FULL TIME 1-2