Baada ya kucheza mchezo wa kwanza wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya AFC Leopard ya Kenya siku ya Simba Day na kuibuka na ushindi wa goli 4-0, leo August 14 2016 Wekundu wa Msimbazi Simba walirudi tena uwanja wa taifa Dar es Salaam kuwakaribisha wakusanya kodi wa Uganda URA katika mchezo wao wa pili wa kirafiki.
Huu ulikuwa ni mchezo wao wa pili kimataifa wa kirafiki chini ya kocha wao mcameroon Joseph Omog aliyeendelea kuchezesha kikosi chake akiwa kakifanyia mabadiliko kwa mchezaji kama Fredrick Blagnon akitokea benchi na Laudit Mavugo akicheza dakika zote 90, huo ni mchezo ambao Simba walitumia kumuaga nahodha wao Musa Hassan Mgosi aliyestaafu soka.
Katika mchezo huo ambao mashabiki wa Simba walijitokeza kuweza kuangalia kama timu yao itaendelea na ushindi mnono kama iliyoupata kwa AFC Leopard, hata hivyo mambo hayakuwa hivyo Simba walitoka sare ya goli 1-1, hiyo ni baada ya URA kufunga goli la uongozi dakika ya 20 kupitia kwa Nkugwa Elkanah, lakini Jonas Mkude alisawazisha goli hilo kwa kichwa dakika ya 32 baada ya kutumia vyema mpira wa faulo uliyopigwa na Mohamed Hussein.
ALL GOALS: Simba vs AFC Leopard August 8 2016, Full Time 4-0