Stori ambayo kwa sasa imechukua headlines kwa wingi ni ile ya tetemeko la ardhi lililotokea eneo la Umbria katikati mwa Italia na kufukia watu chini ya Vifusi.
Imeripotiwa kuwa tetemeko lilisikika katika miji ya mbali kama vile Roma na Italia. Mji wa Roma, baadhi ya majumba yalitikisika kwa sekunde 20. Takribani watu 122 wameripotiwa kufariki kwenye tetemeko hilo.
Sasa hapa millardayo.com & Ayo TV imempata wakala wa Mjiolojia mwandamizi kutoka wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), Gabriel Mbogoni kueleza sababu za Tetemeko la Ardhi.
‘Kwa kawaida Tetemeko La ardhi linatoka Kutokana msukumo wa nguvu za asili zinazosababishwa na mgandamizo kupelekea miamba kukatika sasa hapo ndio Ardhi imepelekea kutikisika ndipo tunasema ndio Tetemeko la ardhi na mara nyingi uwa inatokea kina kirefu cha Ardhi’
‘Lakini pia inaweza ikatokea kina kifupi cha ardhi na inapotokea kwenye kina kifupi ndipo madhara yanatokea kwa nyumba na majengo makubwa pamoja na vifo vya watu’
Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza Geolojia Mwandamizi Gabriel Mbogoni
ULIKOSA ALICHOKIONGEA WAZIRI NCHEMBA BAADA YA KUFIKA ENEO WALIPOUAWA ASKARI POLISI BASI ITAZAME HII VIDEO HAPA