Jioni ya September 3 2016 timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ndio ilihitimisha safari yake ya kuwania kucheza michuano ya mataifa ya Afrika 2017 maarufu kama AFCON, Taifa Stars iliyokuwa Kundi G lenye timu za Misri, Nigeria na Chad ambao walijitoa, imecheza mchezo wake wa kukamilisha ratiba dhidi ya Nigeria Super Eagles.
Taifa Stars ambayo ilicheza mchezo huo wa Kundi G kukamilisha ratiba sawa na Nigeria, imekubali kipigo cha goli 1-0, goli ambalo lilifungwa dakika ya 77 na nyota wa Nigeria anayeichezea Man City ya England Kelechi Iheanacho, hiyo ni baada ya kuishambulia Taifa Stars kwa muda mrefu.
Msimamo wa Kundi G umemalizika hivi Misri ndio kafuzu kucheza #AFCON2017. pic.twitter.com/zbwwH5zD1Y
— millard ayo (@millardayo) September 3, 2016
Mchezo wa kwanza wa Taifa Stars dhidi ya Nigeria ulichezwa September 5 2015 uwanja wa Taifa Dar es Salaam na ulimalizika kwa suluhu ya 0-0, hiki ni kipigo cha 5 Taifa Stars kufungwa na Nigeria katika mechi zake nane walizowahi kukutana, Taifa Stars haijawahi kuifunga Nigeria na wameambulia sare 3 kati ya mara 8 walizokutana.
Goli walilofungwa Taifa Stars na Nigeria
Kelechi Iheanacho, ladies and gentlemen pic.twitter.com/euNNEmmHh6
— OurGirlsWillBeBack (@mcgboye) September 3, 2016
ALL GOALS: Simba vs AFC Leopard August 8 2016, Full Time 4-0