Moja ya headline zilizochukua nafasi katika vyombo mbalimbali vya habari na baadhi ya mitandao ya kijamii ni pamoja na hili la September 10 2016 lilohusisha tetemeko la ardhi katika mkoa wa Kagera na kusababisha vifo vya watu kadhaa huku wengine wakijeruhiwa na hata kupoteza makazi.
Leo September 13 2016 Serikali imeliongelea tukio hilo bungeni Dodoma ambapo Waziri wa nchi Ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa – TAMISEMI George Simbachawene amezungumza kwaniaba ya Waziri mkuu Kassim Majaliwa.
Waziri Simbachawene amesema…>>>’September 10 2016 majira ya saa 9 alasiri mkoa wa Kagera ulipatwa tetemeko la ardhi lenye ukubwa ambalo limesababisha maafa makubwa kwa wakazi wa maeneo hayo‘
‘Idadi ya vifo vilivyoripotiwa katika mkoa huo hadi sasa ni 17, majeruhi 252 ambapo nyumba za makazi zilizoanguka ni 840 na nyumba zenye nyufa ni 1264‘ –Waziri Simbachawene
‘Serikali imeagiza Halmashauri ya Bukoba kufunga kwa muda shule za Ihundo na Nyakato serikali Bukoba kwa kuwa zina hali mbaya‘ –Waziri Simbachawene
‘Serikali inatoa wito kwa wananchi na Kagera na maeneo yote yalioathirika kuwa watulivu na kuonyesha ushirikiano ili kuhakikisha changamoto zilizopo zinatatuliwa kwa kasi ili kupunguza ukubwa wa madhara ya tukio‘-Waziri Simbachawene
Wabunge wameridhia kwa kauli moja kukatwa posho ya siku moja ili ikachangie kwenye msaada wa waliokumbwa na tetemeko la ardhi Kagera.
— millardayo (@millardayo) September 13, 2016
ULIMIS HII RIPOTI YA KWANZA YA MAMLAKA YA HALI YA HEWA BAADA YA TETEMEKO BUKOBA