Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania DK John Pombe Magufuli ameguswa na timu ya taifa ya soka ya bara ya wanawake (The Kilimanjaro Queens) kwa kuandika historia mpya na ya kipekee katika soka la ukanda wa Afrika Mashariki.
Kupitia kwa waziri wa habari, sanaa, utamaduni na michezo Moses Nnauye ameombwa na Rais Magufuli kufikisha salamu za pongezi kwa timu ya Kilimanjaro Queens ambayo jana iliibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya timu ya taifa ya Kenya ya wanawake Harambee Starlets katika mchezo wa fainali ya michuano ya CECAFA Challenge.
“Mh waziri Nape naomba unifikishie pongezi nyingi kwa wachezaji wa Kilimanjaro Queens, shirikisho la soka Tanzania TFF, walimu na viongozi wa timu pamoja na wadau wote waliochangia kuiandaa timu yetu ya taifa ya wanawake ambayo hatimae imepata Ubingwa katika michuano hii mikubwa” >>> Rais Magufuli
Rais Magufuli ameipongeza timu ya Kilimanjaro Queens kwa kutwaa Kombe la CECAFA Challenge kwa mara ya kwanza katika historia. pic.twitter.com/TFLeGuEt4k
— millard ayo (@millardayo) September 21, 2016
Kufuatia Ubingwa huo walioutwaa Kilimanjaro Queens wameweka rekodi ya kuwa Bingwa wa kwanza wa michuano hiyo katika historia, kwani ndio kwa mara ya kwanza imefanyika mwaka huu na wao kufanikiwa kuwa mabingwa hivyo watabaki kuwa na heshima ya kuwa bingwa wa kwanza katika historia.
ALL GOALS: Simba vs AFC Leopard August 8 2016, Full Time 4-0