Baada ya tambo za muda mrefu zilizokuwepo kwa mashabiki wa Yanga na Simba, jioni ya October 1 2016 uwanja wa Taifa Dar es Salaam ilikuwa mwisho wa ubishi kwa mashabiki kuvutana na kutoleana maneno ya kejeli, kwani ndio siku uliochezwa mchezo wa watani wa jadi uliozikutanisha timu hizo za Kariakoo Dar es Salaam.
Huu ni mchezo ambao mashabiki wa Yanga walikuwa na matumaini ya kuwa wataendeleza ubabe wao wa kuifunga Simba kwa mechi zote mbili kama walivyofanya msimu uliopita, huku mashabiki wa Simba waliingia uwanjani wakiwa na matumaini ya kuondoa uteja ambao tayari ulianza kuwazoea kutokana na msimu uliopita kufungwa goli 2-0 katika michezo yote miwili.
Katika mchezo huo ambao ulimalizika kwa sare ya goli 1-1, ulianza kuleta mvutano dakika ya 29 ikiwa dakika 2 tu zimepita toka Amissi Tambwe aipatie goli la uongozi Yanga, goli ambalo nahodha wa Simba Jonas Mkude hakuridhika nalo na kuanza kumzonga muamuzi na kuoneshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja.
Kipindi cha pili kilionekana kuwa kigumu kwa timu zote kutofungana, kwani Simba licha ya kuwa pungufu walifanikiwa kusawazisha goli dakika ya 86 kupitia kwa Shiza Ramadhani Kichuya aliyepiga kona iliyoingia wavuni moja kwa moja na kuufanya mchezo umalizike kwa sare ya goli 1-1.
Msimamo wa #VPL ulivyo kwa sasa baada ya mechi ya leo October 1 2016. pic.twitter.com/KKS852TGzV
— millard ayo (@millardayo) October 1, 2016
GOALS: TP Mazembe vs Yanga August 23 2016, Full Time