October 8 2016 tamasha la mashindano ya ngoma za jadi lililoandaliwa na Naibu spika wa bunge la Tanzania Dk. Tulia Ackson yaliyopewa jina la’Tulia traditional dances festival 2016′ lililofanyika katika viwanja Tandale, Tukuyu mkoani Mbeya kwa siku mbili lilihitimishwa rasmi baada ya kuwapata washindi wake.
Baadhi ya viongozi wa serikali wakiwemo wabunge walishiriki katika tamasha hilo ambalo limelenga kurudisha na kuboresha tamaduni za kitanzania ambapo kwa mara ya kwanza yalishirikisha tamaduni mbalimbali za kutokea wilaya za Mbeya zikiwemo Kyela, Tukuyu pamoja na Rungwe huku mgeni rasmi akiwa ni Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Nape Nnauye.
Nimekusogezea video ya michuano ya burudani ilivyoachiwa….
https://www.youtube.com/watch?v=t2kFC7Q9zio&feature=youtu.be
ULIKOSA HII YA NAIBU SPIKA DK. TULIA KUTANGAZA KUIENDELEZA JADI