Kutoka Shirika la afya duniani WHO leo October 11, 2016 mtu wangu nakuletea taarifa hii kuhusu madhara ya matumizi ya Sukari kwenye nchi nyingi duniani ambayo yamepelekea WHO kuzitaka serikali za nchi husika kuanza kutoza kodi kubwa kwenye vinywaji vinavyotumia sukari, ili kupambana na tatizo la unene uliopindukia maarufu kama Obesity, likisema kuwa kufanya hivyo kutapunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya vinywaji vya sukari.
Mapendekezo haya ya shirika la afya duniani kuhusu vinywaji vyenye sukari, yamekuja wakati huu dunia ikijidhatiti kupunguza tatizo la uzito uliopindukia, ambapo kwa sasa mtu mzima mmoja kati ya watatu ana tatizo hilo.
WHO inasema kuwa, kuna ushahidi wa kutosha kwamba utozaji wa kodi ya ziada kwa vinywaji vinavyotumia sukari kutasababisha kupunguza tatizo na watumiaji wa vinywaji hivyo hasa kwa kuongeza kodi kwa zaidi ya asilimia 20.
Kwa maneno mengine, nyongeza ya asilimia 20 itapunguza matumizi ya unywaji wa vimiminika vya sukari kwa zaidi ya asilimia 20, huku asilimia 50 ya nyongeza ya kodi, kutapunguza karibu nusu yake, shirika hilo limesema.
Wakati huo huo idadi ya watu wanaougua ugonjwa wa kisukari duniani imeendelea kuongezeka tangu mwaka 1980, kutoka watu 108 hadi watu milioni 422 mwaka 2014.
Kwa mujibu wa shirika la habaru la Reuters Ugonjwa wa uzito uliopindukia pamoja na kisukari umesababisha vifo vya watu milioni 1 na laki tano mwaka 2012, huku magonjwa yanayohusishwa na matumizi makubwa ya sukari na kupelekea watu kuugua kisukari ukisababisha vifo vya watu milioni 2 na laki 2.
ULIMISS USHAURI WA WAZIRI KIVULI KUHUSU MSD JUU YA MADAWA? TAZAMA HAPA