Mahakama ya Rufaa Tanzania Arusha leo October 24 2016 ilitarajiwa kutoa uamuzi wa rufaa iliyofunguliwa aliyekuwa mbunge wa Longido Onesmo Ole Nangole lakini hukumu hiyo imeahirishwa hadi pale mkurugenzi wa uchaguzi pamoja na mwanasheria mkuu wa serikali watakapowekwa kwenye rufaa hiyo.
Msajili wa mahakama ya rufaa John Kahyoza ambaye alikuwa akisoma rufaa hiyo ametoa siku 21 kwa upande wa wakata rufaa kurekebisha taarifa yake ya rufaa ndani ya siku hizo.
Awali mahakama kuu kanda ya Arusha ilitengua ubunge wa Onesmo Ole Nangole kutokana na kujaza matokeo ya ubunge kwenye fomu ya udiwani
Katika shauri hilo aliyekuwa mgombea ubunge wa CCM jimbo la Longido Dkt Steven Kiruswa alifikisha mahakamani shauri hilo la kupinga matokeo ya ushindi dhidi ya mbunge wa Longido Onesmo Nangole.
Hukumu ya rufaa ya Onesmo Nangole imeahirishwa hadi pale mkurugenzi wa uchaguzi, mwanasheria mkuu wa Serikal watakapowekwa kwenye rufaa hiyo pic.twitter.com/3sEcgcZuJg
— millardayo (@millardayo) October 24, 2016
ULIKOSA HUU MPANGO WA WAZIRI MWIJAGE KATIKA KUDHIBITI BIDHAA FEKI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI