October 28 2016 Benki Kuu ya Tanzania ilitangaza kuchukua usimamizi wa benki ya Twiga Bancorp kuanzia October 28 2016 baada ya kubaini kuwa ina upungufu mkubwa wa mtaji kinyume na matakwa ya sheria ya mabenki na taasisi za fedha ya mwaka 2006 na kanuni zake.
Sasa leo November 8 2016 benki hiyo imeanza kutoa huduma kwa wateja wake, akizungumza na waandishi wa habari jijini Da es salaam, meneja wa usimamizi wa benki hiyo, Nkano Magina amesema………..
>>>kiuendeshaji, kifedha imeonekana Benki ya Twiga iko vizuri ila tatizo limebaki ni lile lile la mtaji, leo ndio tumefungua tutakuwa tunatoa huduma chache sio zote ili kulinda amana za wateja na huduma zingine zitakuwa zinaongezwa kwa namna tutakavyoiona Benki ya Twiga inavyoendelea.
ULIKOSA HI YA BENKI YA TWIGA KUCHUKULIWA NA BoT? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI