Waziri wa mambo ya Ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba leo November 15 2016 ametembelea makao makuu ya Idara ya uhamiaji Dar es salaam kwa lengo la kuangalia utendaji kazi wao na kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili watumishi na idara kwa ujumla.
#Uhamiaji#Makao#Makuu,leo,Vita dhidi ya uhamiaji haramu iongezwe kwa mbinu shirikishi.#Tatizo la kupungua kwa passports limeisha,zinatolewa. pic.twitter.com/hevPzcCwKK
— Dr.Mwigulu Nchemba (MG) (@mwigulunchemba1) November 15, 2016
Moja ya suala ambalo Waziri huyo amelizungumzia ni pamoja na suala la askari wapya wa uhamiaji ambao walikuwa hawajapata malipo kwa wakati huku maafisa utumishi wakituhumiwa kuchelewesha kupeleka majina sababu waliyoitoa ni kukosekana kwa umeme……
>>>’Mnatoa wapi ujasiri wa kuwaibia mpaka askari, hii siyo hisani kama askari ameambiwa atapewa kiasi hiki siyo huruma ndio anachostahili na kazi anafanya ngumu na sasa hivi mmechelewa mnaona kawaida tu, kesho saambili asubuhi tuonane asubuhi ofisini pale’
VIDEO: Kiwanda cha Uhamiaji kuchapa nyaraka zote za Wizara ya Mamo ya ndani