Kama ilivyoripotiwa awali na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) baada ya kutoridhika na kujiridhisha kuwa mmoja wa wachezaji wa Jamhuri ya Congo-Brazzaville, alikiuka kanuni za mashindano ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17.
TFF ilikata rufaa ya mchezaji Langa-Lesse Bercy katika Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF). Kutokana na rufaa hiyo dhidi ya mchezaji huyo wa Congo Langa Lesse Bercy, CAF iliagiza apelekwe Makao Makuu ya Shirikisho hilo Cairo Misri kwa ajili ya kurudia na kuthibitisha umri wake.
Langa anatakiwa kupimwa kwa kipimo cha MRI (Magnetic Imaging Resonance). kipimo ambacho TFF iliagizwa na CAF igharamie zoezi zima ikiwa ni pamoja na kulipia gharama za usafiri wa mchezaji husika na daktari wake pamoja na kulipia gharama za vipimo.
Kipimo ilikuwa kifanyike leo Novemba 19, 2016 saa 5.00 asubuhi mjini Cairo Misri, ujumbe wa TFF wa watu wanne ukiambatana na madaktari wawili uliwasili mjini Cairo tangu Novemba 17, 2016 ili kuwa shuhuda wa zoezi la kipimo hicho.
Jana usiku saa 5.00 TFF ilipokea ujumbe kutoka CAF kuwa mchezaji Langa Bercy ameshindwa kusafiri kwenda Cairo kwa kuwa yuko katika eneo lililoko vitani eneo hilo halikutajwa, TFF bado inafuatilia na kuhakikisha haki inatendeka.
Imetolewa: TFF
ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0