Ni siku ya saba ya ziara ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ambapo leo November 25 2016 ameanza kwenye wilaya mpya ya Ubungo. Ziara yake amaeanza kwa kuzungumza na watendaji mbalimbali wa manispaa hiyo na haya ndio aliyoyasema kwa watendaji hao.
'Ziko kero nyingi ambazo zimeshindwa kutatuliwa na watendaji tulio nao'-RC Makonda #DarMPYA
— millardayo (@millardayo) November 25, 2016
'Ziara yetu imelenga hasa kwenye uwajibikaji, tunachotaka ni kuona watendaji kwa jinsi mmetekeleza wajibu wenu'-RC Makonda #DarMPYA #UBUNGO
— millardayo (@millardayo) November 25, 2016
'Tutawafahamu watendaji wanaowajibika kupitia wananchi wenyewe'-RC Makonda #DarMPYA #UBUNGO
— millardayo (@millardayo) November 25, 2016
'Sifanyi kazi ili niendelee kufanya kazi, ninafanya kazi ili kukamilisha kazi, ikikamilika hata leo naacha nafanya vitu vingine' -RC Makonda
— millardayo (@millardayo) November 25, 2016
'Sitaki watendaji wanipe majibu ya uongo bora useme sijui, ukinidanganya utakuwa umejiharibia mwenyewe'-RC Makonda #DarMPYA
— millardayo (@millardayo) November 25, 2016
'Tunataka tuwatambue wachapakazi wanaomuwakilisha vizuri Rais Magufuli, na tuwatambue wavivu ambao ni mizigo'-RC Makonda #DarMPYA #UBUNGO
— millardayo (@millardayo) November 25, 2016
'Serikali ina watumishi wengi kuliko ufanisi wa kazi yenyewe, idadi tuliopo tulitakiwa tuwe tumepiga hatua kubwa mno'-RC Makonda #DarMPYA
— millardayo (@millardayo) November 25, 2016
'Tuanze kufikiri nje ya box, mimi na wakuu wa wilaya tunafikisha mwaka mmoja, mpaka sasa tumeichangia serikali zaidi ya Bil 30'-RC Makonda
— millardayo (@millardayo) November 25, 2016
VIDEO; RC Makonda alivyoamuru Mwenyekiti mwingine akamatwe katikati ya mkutano, Bonyeza play hapa chini
VIDEO; Mwenyekiti aliyedaiwa kujiita ‘mungu’ wa Bonyokwa alivyoshtakiwa kwa RC Makonda