Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM imekutana leo Decmber 13 2016 jijini Dar es salaam kwa kikao cha siku moja cha kawaida. kikao hicho kimeongozwa na mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Dkt. John Magufuli
Pamoja na mambo mengine, halmashauri kuu ya Taifa imepokea taarifa ya tathmini ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, baada ya kuitafakari taarifa hiyo haya ni baadhi ya mambo yaliyoamuliwa
'Vyeo ambavyo havikutamkwa ndani ya katiba ya CCM haviruhusiwi, nafasi hizo zimefutwa na hazitakuwepo'-Nape Nnauye #MaamuziCCMNEC
— millardayo (@millardayo) December 13, 2016
'NEC imeagiza iundwe kamati maalumu kuhusu hali ya kisiasa Z’bar, iko tathmini imefanyika lakini NEC haikuridhika'-Nape #MaamuziCCMNEC
— millardayo (@millardayo) December 13, 2016
'Tumeamua kupunguza idadi ya vikao ili tuwe na muda mwingi wa kwenda kwa wananchi'-Nape Nnauye #MaamuziCCMNEC
— millardayo (@millardayo) December 13, 2016
Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kimemteua Humphrey Pole Pole kuwa katibu wa halmashauri kuu Itikadi na Uenezi wa CCM #MaamuziCCMNEC pic.twitter.com/tNGdJph0is
— millardayo (@millardayo) December 13, 2016
'CCM itafanya uhakiki wa wanachama wake ili kujua idadi sahihi ya wanachama kwa kuwa zipo hisia za wanachama hewa'-Nape #MaamuziCCMNEC pic.twitter.com/UNgl1r0NIW
— millardayo (@millardayo) December 13, 2016
'Halmashauri kuu ya taifa ina jumla ya wajumbe 388, idadi ambayo ni kubwa sana hivyo imeamuliwa ipunguzwe na kuwa 158'- Nape #MaamuziCCMNEC
— millardayo (@millardayo) December 13, 2016
Vikao vya kawaida vya halmashauri kuu ya taifa vifanyike kila baada ya miezi 6 badala ya minne isipokuwa itakapohitajika #MaamuziCCMNEC
— millardayo (@millardayo) December 13, 2016
Kwa upande wa sasa imeamuliwa wajumbe wa kamati wawe 24 badala ya 34 #MaamuziCCMNEC
— millardayo (@millardayo) December 13, 2016
'Vikao vya kawaida vya kamati kuu vipunguzwe viwe kila baada ya miezi minne badala ya miwili isipokuwa itakapohitajika-Nape #MaamuziCCMNEC
— millardayo (@millardayo) December 13, 2016
'Vikao vya kawaida vya kamati ya siasa ya mkoa na wilaya vifanyike kila baada ya miezi mitatu badala ya kila mwezi' -Nape #MaamuziCCMNEC
— millardayo (@millardayo) December 13, 2016
'Uhakiki wa wanachama CCM uendane na kutoa kadi mpya za uanachama za kielektroniki ili kuondoa wanachama hewa' -Nape #MaamuziCCMNEC
— millardayo (@millardayo) December 13, 2016
'Kadi za UWT, wazazi na UVCCM zifutwe ili tubaki na kadi za CCM tu'-Nape Nnauye #MaamuziCCMNEC
— millardayo (@millardayo) December 13, 2016
VIDEO: Majibu ya JPM kuhusu kikao cha CCM kufanyikia IKULU, Bonyeza play hapa chini lutazama