Ripoti mpya za shirika la Afya Duniani (WHO) zinasema kuwa ugonjwa wa shinikizo la damu ndio ugonjwa ambao unaathiri watu wengi zaidi barani Afrika huku ikionesha asilimia zaidi ya 10 ya Waafrika wameshapata na ugonjwa huo.
Kwa mujibu ripoti hiyo imeeleza sababu kubwa za kuzidi kuongezeka kwa ugonjwa huo kuwa ni watu kupuuza kufanya mazoezi, kupunguza au kutotumia kabisa matunda angalau matano na mboga kwa siku, matumizi ya tumbaku au sigara na pombe zimetajwa kama njia kuu za kushindwa kupambana na yote yasiyoambukiza ikiwemo Moyo, Kisukari na Kansa.
Ripoti ya Shirika la Afya Duniani (WHO), imeonesha pia robo ya watu wazima kutoka nusu ya nchi za Afrika zilizofanyiwa utafiti wameathiriwa na sababu tatu za hatari zinazoongeza uwezekano wa kuwa na moja au zaidi ya magonjwa mengine hatarishi wakati wa maisha yao.
WHO inaonyesha kuwa wanawake wa Afrika wenye umri wa zaidi ya miaka 45 wako katika hatari zaidi ya kuambukizwa magonjwa haya.
Wakati ambapo matumizi ya tumbaku au sigara na pombe yako kiwango cha chini barani Afrika kuliko sehemu zingine duniani, shinikizo la damu liko katika kiwango cha juu zaidi duniani, na kuathiri karibu nusu ya ya watu wazima barani Afrika.
Kwa mujibu wa WHO, kiwango hicho kinatisha kwa sababu ugonjwa huo unaathiri pole pole na mara nyingi unagunduliwa baada ya miaka kadhaa ukiwa umeshafanya madhara makubwa kwa mgonjwa. Pia ripoti hiyo imeonesha kuwa bara la Afrika ni sehemu pekee watu wanakabiliwa na utapiamlo na fetma.
WHO imeeleza kuwa matatizo haya yanaweza kuzuiwa kwa watu kula vizuri, kunywa kwa kiasi na kufanya mazoezi na endapo tahadhari hizi hazizingatiwi, hali hii inaweza kupelekea kuzigharimu serikali mabilioni ya pesa kwenye matibabu ya wagonjwa wake.
VIDEO: Alice Tupa amekuchambulia Magazeti yote ya leo Decmber 21, 2016. Unaweza kuyatazama yote hapa chini
Unazitaka Breaking NEWS na Stori zote? ungana na Millard Ayo kwenye Facebook Twitter Instagram na Youtube na atakuletea matukio yote ya picha, video na habari iwe usiku au mchana…. bonyeza hapa >>> FB Twitter Instagram YouTUBE