Ikiwa ni siku chache baada ya tozo za maegesho ya magari kupanda jijini Dar es salaam, Meya wa jiji la Dar es salaam Isaya Mwita amekutana na waandishi wa habari leo December 21 2016 kuzungumzia kuhusu wakandarasi ambao wamepewa kazi ya kusimamia maegesho ya magari, bajaji na pikipiki.
Wakandarasi hao hukamata wale wanaovunja sheria kwa kuegesha sehemu ambazo haziruhusiwi, Meya Isaya Mwita akizungumza na waandishi wa habari kavitaja vitu ambavyo wananchi wanatakiwa kuvifahamu kuhusu maegesho ya vyombo vya moto jijini DSM……
1.Wakala atatakiwa kutoa muda wa dakika 60 kabla ya kuchukua maamuzi ya kukamata gari, pikipiki au bajaji iliyovunja sheria
2.Watafanya kazi hii kwa kuzingatia sheria, maelekezo yaliyopangwa pasipo kusababisha bugudha
3.Wakandarasi watafanya kazi hii bila kuvizia magari ya wananchi kwa lengo la kujipatia fedha
4.Watatakiwa kutotoa lugha za matusi
5.Wakala wote wanaokusanya ushuru wa maegesho ya magari DSM wanatakiwa kutumia risiti za kielektroniki kuanzia January 2017
VIDEO: Maamuzi ya Waziri Lukuvi kwa mpima ardhi anayedaiwa kuwa kero kwa wananchi Musoma, Bonyeza play hapa chini kutazama
Unazitaka Breaking NEWS na Stori zote? ungana na Millard Ayo kwenye Facebook Twitter Instagram na Youtube na atakuletea matukio yote ya picha, video na habari iwe usiku au mchana…. bonyeza hapa >>> FB Twitter Instagram YouTUBE